Habari za Punde

Naibu Spika BLW awaaga Madaktari wa Kichina waliomaliza muda wao

 Meneja wa kitengo cha maradhi yasioambukiza Omar Mwalim Omar akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mgeni Rasmi Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma akitoa hotuba kuhusiana na maradhi ya shingo ya kizazi katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar  28/07/2019
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amesema Uchunguzi wa Saratani  ya Shingo ya Kizazi kwa Zanzibar umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kugundua maradhi  mbali mbali ya akinamama na kupatiwa tiba
Amesema wananchi wengi walijitokeza na kufanyiwa uchunguzi  huo na baadhi waliweza kugunduliwa na tatizo hilo.
Hayo aliyasema wakati wa kuwaanga na kuwatunuku vyeti  Timu ya Madaktari kutoka jimbo la Jiangsu nchini China pamoja na  Madaktari na Wauguzi wa ndani ambao wamemaliza mradi wa awamu ya pili wa kutoa huduma ya  upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi Zanzibar.
Amesema wananchi waliofanyiwa uchunguzi katika zoezi hilo  jumla ya watu 5181 walichunguzwa  wagonjwa  72 wamegunduliwa wako katika saratani ya hatua ya awali 15  hatua  ya kiwango cha juu ambao wametakiwa wapelekwe ocean road kwa kupatiwa mionzi  na wagonjwa saba wamefanyiwa upasuaji na 27 wanahitaji kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya mnazi mmoja .
Waziri huyo alisema kupima afya ni jambo la muhimu  kwa kila mmoja wetu  kwani kunasaidia kugundulika kwa maradhi mapema na kupatiwa tiba na kupona kwa haraka .
Aidha alisema saratani ya shingo ya kizazi Tanzania inaongoza kuwa na idadi kubwa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki  takwimu zinaonyesha kati ya watu elfu 35  hupata kensa ya shingo ya kizazi kwa kila mwaka kati ya hao asilimia 20 tu ndio hufika hospitali na  kupatiwa matibabu.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma amewataka wananchi kuzitumia fursa zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za uchunguzi wa afya katika  maradhi mbali mbali ambayo zinatolewa  na wataalamu katika Hospitali ya Rufaa  Mnazi mmoja  .
“Tunatakiwa kufanya uchunguzi wa kiafya hasa sisi akinamama tujichunguze saratani ya matiti ,chingo ya kizazi na hata Tenzi dume kwa akinababa ili  tuweze kujigundua matatizo mapema kuliko maradhi mgonjwa yeshamuathiri  “alisema Naibu Spika
Naibu huyo amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea huduma ya matibabu kwa lengo la kufanikisha Taifa lenye wananchi wenye afya bora .
Naibu Spika aliitaka timu hiyo kuendelee kutoa misaada yao ya huduma za kiafya kwa Serikali ya Zanzibar ili kuweza kuwapatia wafanyakazi wa afya ujuzi wa kitaalamu wa kuweza  kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wao  .
 Nae Mkuu wa Kitengo cha Maradhi Yasiyoambukiza  Omar Mwalim amesema shughuli za upimaji zimekwenda vizuri na madaktari na wauguzi wameweza kuengeza ujuzi wa kazi zao na kufikia malengo yaliyohitajiwa.
Aliitaka Wizara ya Afya kuvungua kitengo maalum cha uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ii kuweza kupungua tatizo hili na kuondoka kabisa .
Kwa upande wa Mratibu  wa Madaktari kutoka China Jasmine Qi Xiaomin  alisema uchunguzi wa maradhi ya saratani ya kizazi kutasaidia kuwafanya akinamama wawe na afya bora na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa .
Pia aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa mapokezi mazuri katika muda wote wa mwezi mmoja wa kutoa huduma kwa wananchi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.