Habari za Punde

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Kanyasu Atoa Nafasi Kwa Wadau wa Utalii Nchini.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti  Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Dayna Saimoni ikiwa ni ishara  ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti  Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Esta Satta  ikiwa ni ishara  ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nhe, Constantine Kanyasu akizungumza na watalii wa ndani walitembelea Msitu asilia wa Magoroto ambao ni kivutio kikubwa cha Utalii wakati walipokusanyika usiku kufurahia ngoma za kabila la wadigo,
Kundi la watalii wa ndani kutoka jijini Dar es Salaam walioungana kwa pamoja na kwenda kutembelea msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa nje  mara baada ya kuwasili katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga
Naibu  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa ndani mara baada ya chakula cha jioni katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Baadhi ya watalii wa ndani na wa nje nyakati za usiku wakifurahia ngoma ya kabila wasambaa iliyokuwa ikitumbuizwa kwa watalii hao.
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa nafasi  kwa Wadau wa Utalii nchini kuwa Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii  upo tayari kupokea ushauri, mapendekezo pamoja na mawazo mapya yatakayosaidia kuchochea na  kuinua idadi ya watalii wa ndani.
Pia, Amewataka watu binafsi, mashirika pamoja na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye sekta ya utalii wasisite ofisi yake ipo wazi kwa mtu yeyote.
"Kwa yeyote atakayetaka kuniona kwa ajili ya kukuza na kuendeleza utalii hasa utalii wa ndani kwangu Mimi pamoja Waziri milango ipo wazi muda wote" alisisitiza Kanyasu.
Hayo ameyasema wakati  alipokuwa akizungumza na Watalii wa ndani wapatao 200 kutoka jijini Dar es Salaam ambao walitembelea katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya kutalii ndani ya msitu wenye kila aina ya vivutio vya utalii likiwemo ziwa la kutengenezwa.
Kundi hilo la watalii wa ndani liliratibiwa na Kampuni ya Dalida Tours and Travel Agency kupitia chini ya Usimamizi wa Mratibu wa safari hiyo , Emma David.
Mhe. Kanyasu amesema moja ya mkakati wa Wizara ni kutaka watalii wa ndani wawe namba moja kwa kutembelea vivutio vya utalii badala ya kutegemea Watalii wa kutoka nje kama ilivyo sasa.
Aidha, Mhe.Kanyasu amesema pia  Wizara yake ipo tayari kupokea na kutoa msaada wa hali na mali kwa mtu au kikundi cha watu kitakacholenga kuhamasisha utalii wa ndani.
''Tunataka akili mpya na mawazo mapya ya namna ya kusukuma na kujenga utamaduni wa watu wetu Wawe wa kwanza kutalii kama ilivyo kwa China'' Alisisitiza Kanyasu
Ameongeza kuwa Idadi ya watalii wa ndani hairidhishi hivyo kunahitajika mkakati wa pamoja katika kuhamasisha utalii wa ndani kwa  Watanzania ili waweze kutembelea vivutio hivyo.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amesema kama nchi haiwezi kuifanya sekta ya utalii kama injini ya uchumi endapo Wazawa wenyewe wataendelea kuwa nyuma huku utalii wa ndani ukiwa na mwitikio mdogo.
" Kama taifa na kwa Mwananchi mmoja mmoja bado hatujaitendea hali sekta ya Utalii ni sekta ambayo haijaguswa hata kidogo ni lazima wananchi wawekeze na wakati huo huo wananchi watembelee vivutio vya Utalii.Amesisitiza Kanyasu
Naye, Emma David ambaye ni Mratibu wa kundi hilo la watalii wa ndani  amesema  wamejipanga kuhamasisha idadi kubwa zaidi ya watalii wa ndani kwa kupitia mitandao ya kijamii ili waweze kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoppo nchini.
''Sisi tumejipanga kutembelea mikoa yote lengo letu ni kuunga mkono jitihada za Wizara katika kuhamasisha Utalii wa ndani, Alisisitiza Emma.
Aidha, Ameishukuru Wizara kwa jitihada inazozifanya za kutengeneza mazingira rafiki kwa watu wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye utalii wa ndani.
Naye, Meneja wa Magoroto,  Jeremia   Mchechu amesema mwitikio wa wa watalii kutoka ndani na nje ya nchi umekuwa mkubwa tangu walipoanzisha eneo hilo kama kivutio cha Utalii na eneo la ziwa ambalo ni la kutengeneza limekuwa kivutio kikubwa cha Utalii.
Amesema watalii wengi wanaofaika katika eneo hilo wamekuwa wakipendelea kupanda milima, kuapnda baiskeli milimani pamoja na kutembelea vijijini kwa ajili ya kujifunza tamaduni ya wakazi wa Tanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.