Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Ameondoka Nchini Kuelekea Nchini Uingereza Kwa Safari Maalum.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Uingereza kwa Safari Maalum, kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Kapteni Silima Haji Haji na Meya ya Manispa ya Magharibi B Unguja Mhe.Maabadi Ali Maulid. 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameondoka nchini leo kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume viongozi mbali mbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd walimuaga Rais Dk. Shein.

Dk. Shein katika safari hiyo, amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.