Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema hana nia wala Adhma ya kugombea Urais wa Zanzibar jambo ambalo siyo kweli na wala hana nia hiyo, amesema kumekuwa na maneno kutoka kwa baadhi ya watu kwamba amekuwa na nia ya kugombea au kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Ujao jambo ambalo siyo kweli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kiongozi wa Banki ya NMB Vicky P. Bishubo alipotembelea maonesho kuangalia bidhaa za mbali mbali katika kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni wa Kituruki waliohudhuria katika maonesho ya kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo
Wazee wa Kijiji cha Kizimkazi wakishiriki kwenye Ngoma ya Kijadi maarufu kama Shomoo wakati wa kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agost 26, 2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment