Habari za Punde

Kikao Cha Kupitia Rasim ya Mkataba wa Utoaji wa Huduma Kwa Wateja.

Mkuu wa Kitengo cha Uperesheni na Huduma za Kibinadamu kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na  Maafa Shaaban Hassan Ramadhani akiuliza suala katika kikao cha kuipitia Rasimu ya Mkataba wa Utoaji Huduma kwa Mteja huko katika Ukumbi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Maruhubi.
Na. Khadija Khamis Maelezo Zanzibar 17 /10/2019 .
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Muhidini Ali Muhidini  amesema michango ya pamoja inahitajika katika kuipitia rasimu ya mkataba wa utoaji huduma kwa mteja ili kuimarisha huduma iliyo bora
Hayo aliyasema huko katika Ukumbi wa Kamisheni ya  Kukabiliana na Maafa wakati wa kikao cha kuipitia Rasimu ya Mkataba wa Utoaji wa Huduma kwa Mteja kwa kushiriki kutoka sehemu mbali mbali  .
Alisema iko haja ya Kuimarisha Mkataba wa utoaji huduma kwa mteja ili uweze kutoa Huduma bora ambazo  zitasaidia kukuza kiwango cha uwelewa kwa wateja wanohitaji kupatiwa Huduma kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa .
Aidha alisema Mpango huo tayari umekwisha kamilika kwa Upande wa Pemba na Unguja  tayari unaendelea katika maeneo ya kaskazini A na B. ili yapatikane maoni zaidi ya wajumbe katika kujadili Mkataba huo
Nae Mkuu wa Kitengo Mipango Utawala na Rasilimali Watu Haji Faki Hamdan alisema huduma ambazo wanazitoa kupitia kamisheni ya kukabiliana na maafa ni pamoja na kusimamia shughuli zote za misaada ya kibinaadamu kwa waathirika wa maafa.pamoja na kutoa tahadhari kwa jamii kutokana na miongozo ya kamisheni
Alisema  muundo wa mkataba huo ni kuitaka  kamisheni  ya maafa kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayotokana na ushauri na mapendekezo ya kamisheni .
Alifahamisha kuwa kuandaa na kutoa mafunzo ya kukabiliana na maafa katika ngazi mbali mbali zikiwemo taasisi za Serikali na binafsi , kamati na wilaya, shehia na jamii kiujumla
Alisema Kamisheni ya Maafa inajukumu la kutunza vituo vya zimamoto na uokozi na vikundi vyengine vyauokozi vilivyomo ndani ya Nchi pamoja na anuani zao kwa ajili ya kurahisisha shughuli za uokozi .
Alifahamisha kamisheni ina jukumu la kuonyesha ramani za maeneo hatarishi yanayoweza kukumbwa na maafa na kutoa ushauri kwa taasisi husika juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa .
Nao washiriki wa kikao hicho wameweza kutoa michango mbalimbali ya kuimarisha Rasimu hiyo ya Mkataba wa Utoaji Huduma kwa Mteja .
Kikao cha kuipitia Rasimu ya Mkataba wautoaji Huduma kwa Mteja ni cha siku moja kilichoandaliwa na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.