Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Abdalla Rashid Abdulla kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa Zanzibar hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Bw.Ali Mzee Ali baada ya kumuapisha kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya Historia na Mambo ya Kale Zanzibar , hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Kjijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliowateua
hivi karibuni.
Walioapishwa ni Bwana
Abdalla Rashid Abdalla aliyeapishwa kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa.
Aidha, Dk. Shein
amemuapisha Bwana Ali Mzee Ali kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Historia
na Mambo ya Kale.
Hafla ya kuwapishwa viongozi
hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid
Viongozi wengine
waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Katibu Mkuu
Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Makatibu
Wakuu.
Wengine ni Mufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan,
Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Viongozi wa Vikosi
vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na
wanafamilia.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment