Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi akishauri umuhimu wa Wataalamu wa Mamlaka ya kuzuia na kuhujumu uchumi kutumia Lugha ya alama katika kutoa elimu kwa Watu wenye Mahitaji Maalum.
Na.Ali Mtwama.OMPR.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Ndugu Shaaban Seif Mohamed amesema Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais itaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kama inavyoelekezwa kisheria ili kuepukana na mwanya wa upokeaji Rushwa na uhujumu uchumu kwa watumishi wa Umma.
Amesema kuwa viongozi wa Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali wana haki na wajibu wa kuendesha na kutumia vyema dhamana walizopewa pamoja na kusimamia wafanyakazi wao kufuata sheria na taratibu za kazi ili kuweza kutoa huduma bora kwa Umma.
Nd.Shaaban Seif Mohamed amesema hayo wakati akifungua mafunzo mafupi ya kupambana na Rushwa yaliyoshirikisha Wakurugenzi wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa pili mafunzo yaliyoandaliwa na maamlaka ya kuzuia na Uhujumu uchumi Zanzibar {ZAECA ) ofisini kwake vuga mjini Zanzibar.
Aidha amesema Ofisi ya Makamu wa Pili kupitia Mtendaji Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya kupambana na kuzuia Rushwa na hujumu Uchumi Zanzibar itahakikisha inapambana dhidi ya uhujumu uchumi pamoja na kutoa mafunzo kwa watendaji wake.
Alisema Mafunzo hayo yatakuwa yakisimamiwa na wataalamu kutoka ofisi ya Utumishi na Utawala Bora kupitia mamlaka ya Rushwa na uhujumu Uchumi Zanzibar ili kuhakikisha Mapambano dhidi ya Rushwa katika Utumishi wa Umma yanaimarika.
Alifahamisha kwamba katika mwaka wa Fedha 2019/20 Ofisi hiyo imetenga bajeti zaidi kwa lengo za kuongeza kasi ya kupambana na Rushwa na uhujumu uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia Rushwa na uhujumu uchumi Ndugu Mussa Haji Ali amesema ipo haja kwa Taasisi za kiserikali kushirikiana katika mapambano ya Rushwa na uhujumu uchumi ili Zanzibar inafikia lengo la kuondokana na tatizo la Rushwa na Uhujumu uchumi hasa katika Taassisi za Umma
“Kila moja wetu kupitia nafasi yake ya Utumishi wa Umma anahaki ya kusimamia wafanyakazi wake ili wanachokihudumia kinakuwa katika msingi ya maadili ya utumishi wa umma kwa kuzuwia mianya ya uhujumu uchumi”. Alisema Mkurugenzi Mussa.
Akizungumzia suala la fomu za maadili kwa viongozi wa Umma amesema kuwa kila mtumishi wa umma hasa Kiongozi ana dhamaan ya ujazaji wa fomu hizo ili kubainisha kiwango cha mali anacho miliki kwa mustakabala wa kuepusha viashiria vya Utowaji Rushwa na uhujumu Uchumi.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameitaka mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu uchumi kutowafumbia macho wale wote wanaofanya vitendo vya uhujumu uchumi kwani kufanya hivyo kunachangia kuzoroteshwa maendeleo yanayokusudiwa kuwafikia wananchi.
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Abdulla Hassan Mitawi ameishukuru mamlaka ya kupambana na rushwa na uhujumu uchumi kwa kuwapatia elimu hiyo watendaji wa Ofisi hiyo na kuahidi kufanya nao kazi pamoja katika nyanya mbalimbali ili kufikia lengo husika.
Nd. Mitawi aliushauri Uongozi na Watendaji wa Mamlaka hiyo kuwatumia wataalamu wa lugha za Alama watakaowasaidia Wananchi wenye mahitaji maalumu ili nao wapate haki hiyo ya elimu ya Mapambano dhidi ya Uhujumu uchumi.
No comments:
Post a Comment