Habari za Punde

Walimu Waadhimisha Siku ya Walimu Duniani Kwa Kuwanya Usafi Kisiwani Pemba.

Na Miza Othman –Maelezo Pemba .
Walimu wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuendeleza usafi katika mazingira yaliyowazunguka ili kujiepusha na maradhi yanayoweza kuepukika hasa katika jamii yao.
Hayo yameelezwa na Kaatibu Tawala Mkoa wa Kusini Pemba  Abdalla Rashid Ali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chake-chake  Rashid Hadidi katika  Kiwanja cha tenisi  wakati alipokuwa akizungumza na walimu hao  mara baada ya  kufanya usafi katika Hospitali ya Chake-chake Kisiwani Pemba.
Amewataka walimu hao kujitokeza mara kwa mara  kuendeleza usafi katika mazingira yaliyowazunguka ili kuondokana na maradhi na kupunguza gharama kubwa za tiba wakati wanapohitaji matibabu.
Hata  hivyo Katibu Abdallah Rashid amesema  wapotayari kushirikiana bega kwa bega katika shamrashamra za kusherehekea  katika sherehe zao hadi kufikia kilele cha sherehe hizo.
Katika Risala yao walimu hao wamesema ndani ya  sherehe zao hutathimini utendaji wa kazi zao kwa mwaka uliyopita pia walimu hao hutoa kiliyochao  mbele ya Serikali kutokana na changamoto zinazo jitokeza kwa walimu na wanafunzi wakati wanapojifunza na kuwafundisha, na kueleza mafanikia yaliyopatikana katika sekta ya Elimu.
Aidha walimu hao wamewashukuru  viongozi  wa Mkoa wa kusini Pemba kwa kuwa wabunifu katika Mkoa wao wanayosimamia ikiwa ni mfano mwema  na ufuwatiliyaji wao wa karibu katika shughuli zao za Serikali ikiwemo sekta ya Elimu.
“Waheshimiwa hongereni sana na spidi mliyoanzia endeleeni nayo hiyo hiyoau zidisheni zaidi, nasi kuko pamoja nanyi” walisema walimu.
Hata hivyo wametoa msemo wao kwa kusema Mwenye macho haambiwi tazama  na asiyejua maana haambiwi maana, kwani ni utamaduni wao wa kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Taifa hasa ili ya Kidato cha Nne na Sita kwa ni imeleta ushindani  wa masomo yao.
Amesisitiza kwa kuseama ushindani huo si kwa wanafunzi tu bali hata Walimu kwa walimu, Skuli kwa Skuli, Wilya kwa Wilaya, hadi Mkoa kwa Mkoa hufanyika na kuwanda utoaji wa zawadi kwani kufanya hivyo kumekuwa chachu katika kuharakisha maendeleo ya kieleimu.
Wameeleza  Wazee wa zamani wanamsemo wao walisema, ukiona vyaelea ujuwe vimeundwa, wakaenda mbali wakasema tena “Mti hawendi ila kwa nyenzo. Kwani kufanya hivyo kunapelekea  matokeo mazuri wanayoyapata wanafunzi wao yanatokana na juhudi kubwa zinzochukuliwa na walimu kuwasimamia, kuwaongoza kuwafundisha wanafunzi hao.
Wamesema kwani ni mwaka wa sita tangu Serikali ya awamu ya saba iingie madarakani chini ya uongozi wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK, Ali Mohammed Shein.
Pia wamepata maendeleo makubwa katika Sekta yao ya Elimu wameyashuhudia yakifanyika ikiwemo kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa,ikiwemo ujenzi wa Skuli mpya za kisasa, mijini na vijijini,ujenzi wa maabara uimarishaji wa miiundombinu katika Skuli utekelezaji wa vitendo wa tamko lililotolewa na Raisi wa kwanza wa Zanzibar jemedsri wa Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na kwamba hata dakhalia sasa hawachangii tena.
“Tunaipongeza kwa dhati Serikali yetu hii kwa namana inavyowajali wanachi wake” walisema.
Kwa kipindi kirefu walimu hao wamekuwa wakikosa ile haki yao ya kisheria ya kupanda madaraja na nyongeza ya kila mwaka ya mshahara kwani changamoto hiyo imekuwa ikiwasononesha na kuwahudhumisha sana kwani imefika wakati sasa maisha ya kambare, hajuulikani mwalimumzoefu katika kazi wala mwalimu mpya anayeanza kazi leo.
“heshima ya kazi ya ualimu imeanza kupotea kutokana na kukosekana kwa hili leo usishangaemwalimu kuwa na mshahara sawa na mwanafunzi wake aliyemsomeha darasani au mwalimu akapitwa na mwanafunzi” walisema.
Kaulimbiu ya siku ya walimu Duniani mwaka huu ni “Vijana na matumainin ya Elimu baadae”.
Walimu wa Zanzibar wanaungana na walimu wenzao duniani kusherehekea siku ya walimu Duniani  Siku hiyo husherehekewa kila ifikapo tarehe 5 Octobar ya kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.