Habari za Punde

Timu ya Vijana ya U-20 Karume Boys Kuwasili leo.Ikitokea Nchini Uganda

NA HAWA ABDALLAH,ZANZIBAR
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya Umri wa miaka 20 Karume boys Leo inatarajia kuwasili visiwani Zanzibar   wakitoka nchini Uganda katika michuano ya CECAFA nchini ya umri huo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  katibu wa shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Mohamed Ali Hilali alisema timu hiyo inatarajiwa  kuwasili majira ya jioni katika uwanja wa ndege wa Abeid karume.
Akizungumzia juu ya matokeo mabaya waliyoyapata timu hiyo ya karume Boys alisema shirikisho hilo lilipeleka timu si kwasababu ya kushindana bali ipo katika mpango wake wa maendeleo wa kuwanyanyua vijana katika umri wao sahihi wa kucheza soka kulingana na mshindano.
Alisema katika kipindi hiki ZFF ipo katika mpango wa kuhakikisha timu zote za vijana zinashiriki mashindano kulingana na umri wao ili kuweza kuondokana na utaratibu uliozoeleka hapo nyuma wa kupekleka vijana ambao baadhi yao hawakuwa na umri sahihi kulingana na mashindano husika.
“ZFF haijashtuka sana na matokeo ya karume boys sisi lengo letu ni kutafuta vijana ambao umri wao upo sahihi, na karume boys ilichaguliwa vijana ambao wote walikuwa chini ya umri wa miaka 20, mpango huu utaweza kupata  hata timu ya taifa ambao wengi wao watakuwa vijana na timu ya karume boys itakuwa ndio timu ya kwanza ya vijana katika mpango wetu huu”Alisema
Timu ya karume boys ambayo ilishinda mchezo mmoja kati ya michezo yake mine iliyocheza licha ya kutolewa katika hatua ya robo fainali  na timu ya Elitria ambayo iliwafunga magoli 5-0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.