Habari za Punde

Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Yatiliana Saini na Kampuni ya Ujenzi ya Advert Construction Limited Ujenzi wa Jengo Jipya la ZRB Pemba.

KAMISHNA wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Kulia Joseph Abdalla Meza, akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji Dhruv Jog, kutoka  Kampuni ya Advent Construction Limited ya Tanzania Bara, juu ya ujenzi wa jengo la Gorofa nne la bodi hiyo litakalogharimu Bilioni 10.6, huku viongozi mbali mbali wa serikali wakishuhudia utiaji saini huo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla katikati
KAMISHNA  wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kulia Joseph Abdalla Meza, akibadilishana mikataba baada ya kutiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji Dhruv Jog, kutoka kampuni ya  Advent Construction Limited ya Tanzania Bara, juu ya ujenzi wa jengo la ZRB Pemba, hafla iliyoshuhudiwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla
KAMISHNA  wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kulia Joseph Abdalla Meza, akizungumza mara baada ya hafla ya utiaji wa saini juu ya ujenzi wa jengo la bodi hiyo Pemba, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Advent  Construction Limited  Ashutosh Jog, akizungumza mara baada ya kutia saini ujenzi wa jengo la ZRB Pemba, halfa iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Gombani.
MWENYEKITI wa Bodi ya Mapato Zanzibar Saleh Saidk Othman, akizungumza wakati wa utiaji saini wa Ujenzi wa jengo la ZRB Kisiwani Pemba, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla
WATENDAJI mbali mbali wa Serikali Pemba wakiongozwa na maafisa wadhamini wa Mawizara mbali mbali, wakishuhudia zoezi la utiaji wasaini Ujenzi wa Jengo la ZRB Pemba, Hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Gombani.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na watendaji wa ZRB, Kampuni ya Advent na maafisa wadhamini Pemba, mara baada ya utiaji saini wa ujenzi wajengo la ZRB Pemba huko katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.