Habari za Punde

Uzinduzi wa Upimaji wa Afya Kwa Wazee Wanaoishi Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akikabidhiwa baadhi ya Vifaa vya Afya kwa Ajili hya Nyumba za Wazee za Welezo na Sebleni na Mke wa Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Bi. Liu Jie, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba ya Sebleni na Welezo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makaazi yua Wazee Sebleni Wilaya ya Mjiniu Unguja, kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar,huduma hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe.Maudline Castico, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji wa Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar.Bi. Fatma Gharib Bilal, Naibyu Waziri.Mhe.Shadya Mohammed na Mkuu wa Wilaya ya Mjini.Bi.Marine Thomas Joe.
WAZEE wa Nyumba ya Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein, akihutubia na kuzindua Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee inayotolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina katika ukumbi wa Sebleni kwa Wazee
MADAKTARI Bingwa kutoka Jamuhri ya Watu wa China, wakitowa huduma ya upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar, wakati wa hafla hiyo, kushoto Dr,Qi.Ming akitowa huma ya upimaji wa presha kwa.Bwa.James Ngagu na kulia Dr.Qiu Honghe akitowa huduma hiyto kwa Bi. Pili Maig, baada ya Uzinduzi huo uliofanywa na Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) iliofanyuika katika ukumbi wa Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja
MKE wa Balozi Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Zanzibar.Bi.Liu Jie akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Sebleni na Walezo Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa nyumba za wazee sebleni na Madaktari wa Jamuhuri ya Watu wa China

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.