Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui akizungumza na waandishi ofisini kwake ambao hawapo pichani waliotembelea hifadhi hiyo kuhusu vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui akiwaonyesha waandishi wa habari bwawa la Dindira lililopo hifadhini humo ambalo linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji ambao walitembelea
bwawa la Dindira lililopo hifadhini humo ambalo linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji
HIFADHI ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro imeeleza kwamba watatumia mavuvuzela na tochi zenye mwanga mkali kuwafukuza wanyama wanaovamia makazi ya wananchi wakiwemo Tembo na kuwarudisha kwenye hifadhi.
Hayo yalisemwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Abeli Mtui wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea hifadhi hiyo.
Alisema kwamba watashirikiana pia na baadhi ya taasisi binafsi ambazo zimebuni mbinu za kuwafukuza wanyama hao ikiwemo la wakulima kufundishwa namna ya kuweka uzio wa mabati ambayo yanayopiga kelele na imesaidia kwa asilimia kubwa.
Kamishna huyo Msaidizi wa Uhifadhi alisema wamefanya jitihada zote huku akitoa wito kwa wananchi wazingatie na wanaona ufumbuzi wa mkubwa ni yale maeneo ambayo yalikuwa ni mapitio ya wanyama kufanya matumizi bora ya ardhi,rafiki yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yake ya kuchunga ili kupunguza mgongano wa kuharibu mazao.
“Kikubwa ni kutenga au kufanya matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji yale maeneo yenye historia ya kupita wanyama watu wayapangia matumizi ambayo ni rafiki au matumizi yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yawe ya kuchungia ili kupunguza mgogano wanyama kuharibu mazao”Alisema
Aidha alisema kwamba wana matumaini makubwa na kuna mikakati wanaoiweka ili wasaidiane na viongozi wa vijiji katika kukamilisha mipango bora ya matumizi ya ardhi ili maeneo yaliyonekana ni mapito ya wanyama yaweza kufanyiwa matumizi mazuri yanayoendena na uhifadhi wa wanyama pori pia na matumizi ya mifugo kama malisho.
Alieleza pia kwamba hifadhi hiyo ni moja kati ya hifadhi ambayo inapakana na Hifadhi ya Tsavo West ya Kenya na katika mfumo wa ikolojia ya savo mkomazi kwa upande wa Kenya ndio eneo lenye idadi kubwa ya Tembo kwa mujibu wa sensa miaka iliyopita kwenye huo mfumo kulikuwa na tembo 23000 .
Alisema na mwaka 2014 hesabu ilifanyika na walionekana tembo 60 na wao wamefanya sensa mwaka huu wakati wa kiangazi wamepata tembo zaidi ya 1000 ina maana idadi kubwa ya tembo wameongezeka na hao tembo ni kwa sababu hawana mipaka wanaotembea kwenye mfumo wa ikolojia na kipindi hicho wamekuwa na tembo wengi ambao wamekuwa wakipita kwenye makazi ya watu.
“Hili linatokana na kwamba mara nyingi tembo eneo ambalo amepita miaka ya zamana anatabia ya kupita tena kilichoonekana kwenye kipindi cha kiangazi mapito ambayo yalikuwa ya tembo wanapita watu wamevamia na kuweka makazi hata madhara makubwa yametokea”Alisema.
Hata hivyo alisema kwamba changamoto kubwa ni watu wamelima karibu na hifadhi huku wakiwa hawajaacha hata mita moja na ndio changamoto inapelekea kuwa rahisi tembo kuingia kwenye hayo maeneo na mashamba na kufanya uharibifu mkubwa.
Naye kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi katika Idara ya Utalii hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Benard Mgina amesema hali ya utalii wageni wamezidi kuongezeka kwa sababu ukiangalia takwimu 2009 hadi 2010 wageni 854 wametembela hifadhi wageni wa nje walikuwa ni 419 na wa ndani 435.
Aliema utaona kuna utofauti mkubwa sana vile vile ulkiangalia hesabu kutoka mwaka 2009 /2010 kwenda 2018 hadi 2019 kuna tofauri kwa sababu 2009 /2010 ilikuwa wageni 854n lakini 2018/2019 wamepokea wageni 2930.
Afisa Mwandamizi huyo wa Uhifadhi wa Idara ya Utalii alisema kwamba wageni ambao wamepokelewa kwa mwaka 2018/2019 kati yao wageni 728 kutoka nje na 2200 walikuwa wageni wa ndani kuna utofauti mkubwa sana.
No comments:
Post a Comment