Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Mradi wa Ufugaji wa Kuku wa Mayai.

Eneo linalotayarishwa kwa ajili ya Mradi wa Shamba la Kuku wa Mayai liliopo katika Kijiji cha Kandwi, Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja litakaloendeshwa na Kampuni ya Wazawa ya Modern Agricultural Product.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Modern Agricultural Product Bwana Mahir Abdulrahman kwenye eneo linalotayarishwa kuwa shamba la Kuku wa Mayari hapo Kandwi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Modern Agricultural Product  Bwana Mahir Abdulrahman akimueleza Balozi Seif mipango ya uendelezaji wa shamba la Kuku Kandwi litakalotoa ajira na kuongeza mapato ya Taifa.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akimzikiliza Mkuu wa Mradi wa Shamba la Kuku wa Mayai la Kandwi Ndg.Jaffar Hussein akielezea mikakati ya Taasisi yake katika uamuzi wa kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Nadir Abdul-latif akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, alipotembelea mradi wa Ufugaji wa Kuku wa mayai 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.