Habari za Punde

Wananchi wa Vijiji Vya Mpapa na Umbiji Wilaya ya Kati Unguja Wananufaika na Mradi wa Tasaf Kupuguza Kaya Maskini Kwa Kilimo cha Vitunguu Maji

Wakulima wa Kaya Maskini waVijiji vya M,papa na Umbuji wakiendelea na zoezi la uvunaji wa Vitunguu kwenye Mashamba waliyolima wakipata baraka ya uvunaji huo kutoka Viongozi wa Mfuko wa Tasaf.

Wananchi wanaonufaika na mpango wa kupunguza Kaya maskani (TASAF) wametakiwa kubuni zaidi miradi mbali mbali itakayowasaidia kujiingizia kipato sambamba na kuonddosha umaskini katika shehia zao ili kufikia lengo la Serikali la kuwasaidia wananchi wake.
Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Ndugu Khalid Bakari Hamrani alieleza hayo katika zoezi maalum la uvunaji wa vitunguu maji kwa wananchi wanaonufaika na mpango wa kaya maskini katika Vijiji vya Mpapa na Umbuji wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Khalid aliwapongeza wananchi hao kwa jitihada zao za kuendeleza mpango wa mradi waliounzisha katika mazingira magumu ambapo uendelezaji wa mpango huo ulikua chini ya uwangalizi wao wenyewe jambo ambalo linasisitizwa na viongozi wakuu kuwa wananchi waiendeleze miradi wanaoachiwa ili iwaongezee tija na kipato.
Alisema ni jambo linalotia moyo kwa viongozi wa serikali kwa kuona kwamba wananchi wamekuwa na muuamko wa kulima na kuzalisha bidhaa ambazo awali hazikuwa zikizalishwa Zanzibar  na badala  yake kujengeka kwa dhana ya kwamba bidhaa za aina hiyo hukubali katika aridhi maalum pekee lakini kwa sasa kumeshuhudiwa kwa wimbi kubwa la uzalishaji wa bidhaa za aina hiyo hapa Zanzibar.
Aidha Mkurugenzi Khalid  aliwahakikishia wanakaya hao kuwa hivi karibuni Ofisi ya TASAF itaanza rassmi zoezi la kuwalipa wananchi fedha zao kabla ya mpango mpya wa TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili hajaanza utekelezaji wake.
Akielezea faraja yake mwanachi kutoka katika kaya Maskini kijiji cha Mpapa Bi zainab Hassan Ameir alisema kupitia mradi huo wa kilimo cha vitunguu maji kinawawezesha kujikimu kimaisha sambamba na kufikia azma ya serikali katika kupambana na umaskini kwa wananchi.
Bi  Zainab alisisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar sio maskini ila jambo la msingi linalohitajika kwao ni kupatiwa elimu pamoja na usimamizi imara na amewaomba wananchi wenzake katika shehia nyengine kuiga mfano wao kwa kuanzisha miradi kama hiyo katika sehemu zao ili waweze kunufaika.
Nae Mratibu wa TASAF Ungunja Ndugu Makame Haji Ali alisema serikali kupitia Ofisi ya (Tasaf) itaendeleza mpango wake wa kuwafikia wananchi katika shehia zote Unguja na Pemba kwa kuwapa elimu sambamba na kuwapa moyo juu ya uendelezaji wa miradi yao walioianzisha.
Alifafanua kuwa, kutokana na matokeo mazuri yaliopatikana katika zoezi la ulimaji wa vitunguu maji katika ardhi ya Zanzibar Ofisi yao itaangalia uwezekano wa kufanya majaribio ya kulima mbatata ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ubunifu kwa walengwa wa mpango huo.
Mratibu Makame alitoa wito kwa Maafisa ugani waliopo katika kila wilaya kuweka utaratibu wa kuwapitia wakulima na wafugaji kwa kuwasikiliza changamoto zao zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi ili walengwa hao waweze kupata faida zaidi juu ya miradi wanayoiendeleza.
Kwa upande wake Kiongozi wa wanakaya Maskini wa kijiji cha Mpapa Bw. Abdi Mussa Khamis alisema mradi wa ulimaji wa Vitunguu Maji umekuwa ukiwaingizia tija kutokana na uzalishaji kuongeza kila kipindi cha mavuno  na kupata vitunguu vyenye ubora lakini changamoto kubwa inayowakabili ni mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na kubadilika kwa miongo.
“Niseme tu ulimaji wa vitunguu maji hauhitaji mvua nyingi sasa kwa msimu huu katika kipindi cha mwishoni mvua za vuli zimetuathiri kwa namna moja au nyengine” Alieleza Bw. Abdi.
Mkuugenzi Uratibu wa shughuli za Serikali SMT na SMZ Nd. Khalid Bakar Hamran Kati kati aliyevaa shati ya drafti akijumuika pamoja na Wanakaya Maskazni wa Vijiji vya Mpapa na Umbuji kwenye zoezi la uvunaji Vitunguu Maji.
Mmoja kati ya Wana Kaya Maskini akiwa makini katika zoezi la Uvunaji Vitunguu akihakikisha bidhaa hiyo inakuwa katika kiwango itapoingizwa sokoni.

Mkurugenzi Khalid na Wasaidizi wake wakiwa makini katika ushiriki wao kwenye zoezi la Uvunaji wa Vitunguu hapo katika Kijiji cha Mpapa na Umbuji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.