Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Cheti Mwanafunzi wa Skuli ya Fat-hi Internation Community ilioko Shangani Zanzibar, baada kumaliza masaomo yake ya Awali ya Maandalizi wakati wa hafla hiyo
Na.Rashida Abdi/Kassim Salum.OMPR.
Wazazi na walezi nchini wameshauriwa kutenga sehemu ya muda wao kwa kufuatilia nyendo na tabia za watoto wao ili kuhakikisha kile wanachowafunza kinasimama katika maadili mema.
Kufanya hivyo kutasaidia kujenga Taifa imara na shupavu la hapo baadae sambamba na kuwaepusha watoto kutumbukia ndani ya wimbi lililokithiri hivi sasa la udhalilishaji linaloiathiri jamii.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo katika shughuli ya maghafali ya kwanza ya Skuli ya FAT-HI International Community iliopo Shangani ilioambatana na zoezi la kuwakabidhi vyeti na kuwapongeza wanafunzi waliomaliza ngazi ya Maandalizi { KG-II}.
Mama Asha alitumia fursa hiyo kwa kuwashajiisha na kuwasisitiza wazazi kutenga muda wao kwa kuchunguza tabia za watoto wao zitakazowasaidia kugundua mabadiliko yoyote mabaya yaliyowazunguuka na kwa haraka kuyapatia ufumbuzi unaostahiki.
Aliwaeleza wazazi na walezi kuwa elimu ina mchango mkubwa katika kujenga mustakabali wa maisha ya watoto. Hivyo kuna kila sababu kwa wazazi kutumia jitihada zao zote katika kuwarithisha Elimu Watoto wao ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Mke huyo wa Makamu wa pili wa Rais aliwapongeza Waanzishi wa Skuli binafsi Nchini kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kuinua kiwango cha elimu bila ya kujali ukubwa wa gharama wanazozitoa kwa lengo la kuwafinyanga watoto.
Akisoma Risala Mwalimu wa skuli ya FAT,HI INTERNATIONAL COMMUNITY Sheha Ngweshani alisema skuli hiyo imepata mafanikio makubwa kutokana na watoto wanaosoma katika skuli hiyo wana uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuhesabu sambamba na kuwajenga wanafunzi katika silka na Desturi za Mzanzibari.
Mwalimu Sheha Ngweshani alimueleza Mama Asha kuwa ingawaje yapo mafanikio yaliofikiwa lakini bado inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo kukosekana kwa vifaa kama vile Fotokopi na kompyuta vifaa ambavyo vinakwenda sambamba na ulimwengu wa sasa wa sayansi na Teknolojia.
Nae Naibu katibu mkuu taaluma kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Madina Mjaka Mwinyi alisema ushirikiano unahitajika baina ya wazazi, walezi na walimu katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira wezeshi kwani kufanya hivyo ndio njia pekee ya kuwajenga watoto wakiwa katika hatua ya awali.
Alifafanua kwamba Serekali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa elimu kuanzia ngazi Maandalizi, Msingi na Sekondari, hivyo skuli Binafsi nazo zina wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo.
Katika shughuli hiyo ya Maghafali Mama Asha aliahadi kuchangia vifaa kama vile Kopyut na Printa ili kutatua miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo ya Fat-Hi International Comuunity.
Wanafunzi wa Skuli ya FAT-HI International Community wakiimba wimbo katika shughuli ya maghafali ya kwanza ya Skuli ya yao ilioambatana na zoezi la kukabidhiwa vyeti.
Mke wa Makamu wa Pili wa Raius wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza katika shughuli ya maghafali ya kwanza ya Skuli ya FAT-HI International Community iliopo Shangani hapo Mazson Hoteli.
Mke wa Makamu wa Pili wa Raius wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza katika shughuli ya maghafali ya kwanza ya Skuli ya FAT-HI International Community iliopo Shangani hapo Mazson Hoteli.
Naibu katibu mkuu taaluma kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Madina Mjaka Mwinyi akisisitiza umuhimu wa Skuli Binafsi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika Sekta hiyo muhimu.
Baadhi ya Wazazi na Walezi walioshiriki na kuhudhuria shughuli ya maghafali ya kwanza ya Skuli ya FAT-HI International Community iliopo Shangani.
No comments:
Post a Comment