Habari za Punde

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAWAONYA WATUMISHI WA UMMA WAZEMBE PEMBA

Katibu wa Halmashari Kuu ya Taifa ,Itikadi na Uenezi Ndg. Hamphrey Polepole akizungumza Wanachama wa CCM Tawi la Majenzi  wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi na kulifungua Tawi hilo akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba.

Akizungumza katika kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Zanzibar, Ndugu Humphrey Polepole Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi kinawaonya Watumishi wa Umma wazembe, wanaochelewesha maendeleo ya Watu Pemba Zanzibar.

Akifafanua suala hilo Ndugu Polepole amesema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Dk. Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar bado wapo baadhi ya Watumishi wa Serikali wazembe wanaokwamisha kazi ya Serikali jambo ambalo linaweza kuteteresha heshima ya Chama katika Jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.