Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Mussa Sima amesema Serikali imeboresha Kanuni za Usimamizi Elekezi wa Mazingira ili kurahisisha na kuharakisha utoaji wa vibali vya tathmini ya mazingira.
Sima ametoa kauli hiyo jana bungeni jijini Dodoma
wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Biashara na Viwanda ya kipindi cha
Julai hadi Desemba 2019 ambayo pamoja na mambo mengine ilizungumzia urasimu wa kutoa vibali.
Alisema kuwa kupitia maboresho hayo sasa wataalamu hao wanaotambuliwa na Baraza
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) sasa utendaji kazi wao utaboreka kwa kuwa kipengele
cha kanuni hizo kitawabana wafanyaekazi kwa ueledizaidi.
“Hili jambo tumelichukua kama lilivyo ili sasa twende tukakae na wataalamu wetu tukaweke njia sahihi kuondoa urasimu na tunatambua tumebadilisha kanuni lakini
pia tunatambua katika suala la
vibali leo tunatoa vibali vya muda mfupi ndani ya siku saba mtu anapata kibali wakati anasubiri kibali
cha
tathimini ya mazingira ambacho kinachukua muda mrefu na ndio maana inawezekana wawekezaji wanaona kama kuna urasimu,”
alisema.
Kwa upande mwingine kuhusu udhibiti wa biashara ya vyuma chakavu Naibu Waziri aliwaondoa hofu wafanyabishara wa vyuma chakavu kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara za Fedha na Mipango,
Viwanda na Biashara pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha tunalinda miundombinu isiharibiwe.
No comments:
Post a Comment