Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Ahakiki Taarifa Zake Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar leo 29-2-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Kituo cha Kujiandikisha Wupiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja kwa  kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar, (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud. Hafla hiyo imefanyika leo 29-2-2020
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika foleni akisubiri zamu yake katika zoezi la Uhakiki wa taariza zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar, katika Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo, 29-2-2020,  (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe Jaji.Hamid Mahmoud na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg Thabit Idarous Faina
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimpa Kiatambulisho cha Kura Mkuu wa Kituo cha Kujiandikisha Wapinga Kura Skuli ya Msingi Kibeli Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini, Bi. Salma Abdull Mussa, kwa ajili ya kuhakikiwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihakiki Taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar, na Afisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg. Salum Abdulrahaman Nadhif, alipofika Kituo Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo 29-2-2020, (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa  risiti na Afisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg. Salum. Abdulrahaman Nadhif, baada ya kumaliza kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar , katika Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo, 29-2-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja , akisuburi Kitambulisho chake cha mpiga kura baada ya kuhakikiwa na Mkuu wa Kituo cha Kijiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja.Bi.Salma Abdulla Mussa

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya Kati Unguja leo. 29-2-2020. 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihakiki Taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  Zanzibar, alipofika kuhakiki taarifa zake katika Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo, akifanyika uhakiki na Afisa wa (ZEC) Bi. Mwashamba Rashid Abuu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitoka katika Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja baada ya kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, baada ya kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar, katika Kituo cha kujiandisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja  leo,29-2-2020, (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) Mhe. Jaji. Hamid Mahmoud na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.