Habari za Punde

TIRA Imewaomba Wananchi Kuwac na Utaratibu wa Kukata Bima Ili Kujinusuru na Maafa.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo Zanzibar..
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewaomba wananchi kuwa na utaratibu wa kukata bima ili kujinusuru na majanga ya maafa pale yanapotokezea na kupata maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Uendelezaji Soko la Bima Tanzania  Salum Yungwa huko katika Ukumbi wa ZSSF  Kariakoo wakati alipokuwa akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa Bima kwa wananchi kwenye mali zao na upande wa kilimo amesema jamii iwe na mwamko wa kukata bila ili kunusuru mali zao.
Amesema iwapo jamii itakuwa na utaratibu wa kukata bima kwa ajili ya mali zao ikiwemo vyombo vya moto, nyumba au mashamba itaweza kufaidika kuzilinda mali  na majanga pale yanapotokea.
Amefahamisha kuwa mwananchi yoyote anaekata bima lazima utoe taarifa za ukweli ili kuweza kupata haki yako pale unapofikwa na majanga na kuepuka hasara.
Meneja huyo amewasihi baadhi ya wananchi wale wenye tabia ya kununua mali mikononi mwa watu kubadilisha jina la mmiliki na kukikatia bima ili kuepuka usumbufu wakati linapotokea tatizo ili kuweza haki yako.
“Natoa tahadhari kwa wale wanaonunua vyombo vya moto au shamba au nyumba ikiwa wamekatia bima wewe ubadilishe usitumie bima ile kwani ukipata hasara hutambulikani na hutolipwa epuka kufanya hivyo”,alisema Meneja Salum.
Aidha Meneja huyo amewataka wananchi kupatiwa elimu juu umuhimu wa kujiunga na bima  kwani ina faida kubwa pale unafikwa na majanga mbalimbali na kuweza kulipwa fidia ya mali yako iliyopotea.
Nae Meneja wa Mamlaka ya Bima Ofisi za Zanzibar Mohamed Khamis Ameir amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha jamii na kuweza kutambua umuhimu wa bima na jinsi inavyoweza kukusaidia wakati wa majanga yanapotokea.
Wakichangia washiriki wa mafunzo hayo wameomba kutolewa elimu kwa jamii na hasa vijijini ambapo wengi wao  hawana utamaduni wa kukata bima hivyo itasaidia kuinua kwenye kilimo  na kujinusuru na majanga pale maafa yanapotokea ikiwemo kuunguliwa na mashamba yao na madhara mengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.