Habari za Punde

Masauni-Polisi zingatieni Misingi ya Sheria kudhibiti Uhalifu

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo ameahidi kupanga bajeti itakayosaidia kupambana na changamoto mbalimbali kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu  unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Ufunguzi wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akitoa taarifa ya ulinzi na usalama kwa nchi nzima mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),muda mfupi kabla ya naibu waziri kufungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi,kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni baada ya kuwasili Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay kufungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu.                                                                                                                   
Serikali imelitaka Jeshi la Polisi kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au matendo ya uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Machi 16,2020 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Napenda kuwapongeza Jeshi la Polisi chini yako(IGP Sirro),kwa kufanikiwa kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya,ajali za barabarani na uhalifu mwingine ambao hapo nyuma wote tulishuhudia ukiwa umeoata mizizi ila napenda kutoa angalizo kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu mdhibiti viashiria vya uhalifu au matendo ya uhalifu kwa kufuata misingi ya sheria ili tuweze kupita kwa amani na salama katika kipindi hicho” alisema Masauni
Akizungumza katika kikao hicho cha baraza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro alisema wao kama jeshi wanaishukuru serikali na wamejipanga kibajeti kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi
“Kwa kiasi tumefanikiwa kutengeneza bajeti itakayochochea usalama wa raia na mali zao,bajeti iliyoandaliwa itasaidia kutatua changamoto na kwa kuwa kila uchaguzi una changamoto zake sisi tumejipanga na tunazichukua chgangamoto kama fursa” alisema IGP Sirro
Watumishi hao wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi wanakutana katika kikao hicho lengo ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/2020 na Rasimu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2020/2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.