Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud Awapongeza Wanafunzi Waliofanya Vizuri Mitihani Yao ya Darasa la Sita Skuli ya Msingi Mchangani Wilaya ya Kati Unguja.

Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mchangani Wilaya ya Kati wakiimba na kucheza katika Sherehe ya Kuwapongeza Wanafunzi wa Skuli hiyo waliofaulu Michipuo, Huko Uwanja wa Skuli ya Msingi Mchangani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Zawadi Baadhi ya Wanafunzi waliofaulu Michipuo kutoka Skuli ya Msingi Mchangani katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Zawadi Baadhi ya Wanafunzi waliofaulu Michipuo kutoka Skuli ya Msingi Mchangani katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Zawadi Baadhi ya Wanafunzi waliofaulu Michipuo kutoka Skuli ya Msingi Mchangani katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Zawadi Baadhi ya Wanafunzi waliofaulu Michipuo kutoka Skuli ya Msingi Mchangani katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi hao.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mchangani waliohudhuria Sherehe ya Kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Michipuo wa Skuli hiyo hafla iliyofanyika Skulini Hapo.
Picha na Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar.
Na  Mwashungi Tahir   Maelezo Zanzibar.
Serikali ya Mkoa wa Kusini Unguja imeahidi kuondosha changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Skuli ya Mchangani wanapoingia sekondari kufuata elimu kwa masafa marefu.
Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud wakati alipokuwa akizungumza na walimu na wanafunzi kwenye sherehe za kuwapongeza wanafunzi waliofulu mchipuo wa darasa la sita huko katika Skuli ya Mchangani msingi Wilaya ya Kati.
Amesema kutokana na usumbufu unaowapata wanafunzi hao Serikali ya Mkoa huo itahakikisha inalisimamia suala hilo kwa lengo la kuondosha changamoto hiyo ya kufuata elimu ya sekondari kwa masafa marefu.
Aidha amewapongeza wanafunzi hao kwa kuweza kufaulu michipuo na kuingia madarasa ya sayansi na lugha ambayo imeweza kuleta faraja kwa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuwa matokeo hayakuwa mazuri katika skuli nyengine .
Hivyo amewaomba walimu wazidishe juhudi zaidi kwa kupasisha wanafunzi kwa wingi ili maendeleo ya elimu yazidi kupatikana ndani ya Mkoa huo.
Pia amewanasihi wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwapa watoto kazi nyingi za majumbani ili  wawe na muda mwingi wa kujisomea ili waweze kufanikiwa mitihani yao ya michipuo.
“Nawasihi  wazazi na walezi kuwapunguzia kazi watoto wao za majumbani  ili waweze kupata muda muafaka  wa kujisomea na kupata mafanikio mazuri”, alisema  Mh Ayoub.
Hata hivyo amewataka walimu wa skuli nyengine kuwafuata walimu wa Skuli ya Mchangani wakae pamoja na kupeana mawazo ili na wanafunzi wapate na wao mafanikio mazuri kwani tayari washaonyesha njia za maendeleo.
Nae Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mchangani Sharif Suleiman Amour amesema kutokana na ufaulu wa wanafunzi hao skuli hiyo imeweza kuwa ya mwanzo kwa Mkoawa Kusini Unguja  na Wilaya.
Akielezea changamoto amesema skuli wakati wa kipindi cha mvua imekuwa na tatizo la barabara hadi kufika watoto kushindwa kwenda skuli na kukosa masomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamai ya Skuli ya Msingi ya Mchangani Ali Ahmada aweomba  Serikali ifanye juhudi za kuwasogezea skuli ya secondary karibu kwani wanafunzi wanafata masafa marefu kilomita tisa kwenda nne na nusu na kurudi na pia njia hatarishi .
Jumla ya watoto saba wa Skuli ya Mchangani Mchipuo Msingi ya Mchangani wamefaulu wakiwemo wanawake wanne na wanaume watatu.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed alifanya ziara ya kuwakagua wagonjwa ndani ya Mkoa huo akiwemo Mzee Abasi Kombo Vuai mkaazi wa Ndijani Mseweni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.