Habari za Punde

Pasaka yafutwa mwaka huu kwa kuwepo maradhi ya Corona

NA MWAJUMA JUMA
CHAMA Cha Soka Wilaya ya Mjini Unguja kimeghairisha tamasha la michezo ya pasaka yaliyokuwa yafanyike kuanzia April 10 mwaka huu.

Hayo yamethibitishwa na mratibu wa tamasha hilo Ali Abdalla Hassan alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwao Amaan mjini hapa.

Alisema kuwa tamasha hilo ambalo hufanyika kwa zamu kila mwaka na msimu huu wanamichezo wa zanzibar walikuwa ni zamu yao kusafiri na kwenda jijini Dar Es  Salaam na Mikoa mengine ya bara ambapo safari hiyo itakuwa mwakani.

Alisema kuwa kutokana na miripuko wa maradhi Corona Covid 19 safari hiyo imesitishwa na mwendelezo safari utakuwa mwakani .

"Tutaenda kwenye tamasha hili mwakani na tutawajuulisha wenzetu kuwa mwaka huu hatutakwenda na roho zikifika roho tutaenda mwakani", alisema.


Alisema kuwa kwa pamoja kabla ya kutoa maamuzi hayo uongozi wa chama hicho ulikutana na viongozi wa vilabu na mashirika ambao wameorodhesha kushiriki tamasha hilo na kuamuwa kwa mwaka huu wasitishe Hadi hapo mwakani.

"Tulikaa kikao na viongozi wote na kikubaliana mwaka huu tusiende kutokana na uwepo wa Corona na safari yetu ifanyike mwakani", alisema Hassan.

Hivyo alisema kuwa hatua inayofata ni kila mmoja kuchukuwa juhudi za kuwasiliana na mwenyeji wake ili kumpa taarifa hiyo.

Aidha alisema kuwa kutokana na hali hiyo uongozi huo wa ZFA mjini utakutana na mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatibu ili kumpa taarifa hiyo kwa kuwa yeye ndie msimamizi mkuu wa tamasha hilo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.