Habari za Punde

Wanafunzi wa Skuli za Sekondari Zanzibar Watakiwa Kutumia Serekali za Wanafunzi Kuibua Changamoto Zao.

Na.Takdir Swaleh -Maelezo Zanzibar.
Wanafunzi wametakiwa kuzitumia Serikali za Wanafunzi kuibua changamoto zinazowakabili na kuzipeleka sehemu husika ili zipatiwe ufumbuzi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Sekondari Jangombe Bw. Mgeni Mussa Haji wakati alipokuwa katika sherehe za kumuapisha Raisi wa Skuli hiyo.
Amesema matatizo kama vile ya Utoro,Mporomoko wa Maadili na baadhi ya Waalimu kutoingia Madarasani ipasavyo yanaweza kuondoka iwapo Serikali hizo zitafanya kazi kwa uhakika.
Aidha Bw. Mgeni amewaomba Viongozi wa Serikali hiyo kufanya kazi kwa uadilifu wa kuwatumikia Wanafunzi na kushirikiana na Waalimu katika kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Jangombe Abdallah Kheir Hassan ameitaka Serikali ya Wanafunzi kuweka Mahusiano mazuri baina ya Waalimu na Wanafunzi ili kuweza kuleta maendeleo katika masomo.
Nao Viongozi wa Serikali hiyo wameahidi kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo kuwapatia Vipande maalum Wanafunzi wanaokaa mbali ili kuepukana na kupata adhabu za kuchelewa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.