Habari za Punde

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani "NURSING NOW"

Wauguzi na wakunga wakiwa kwenye mandamano ya siku ya Wauguzi (Nursing Now) yaliyofanyika viwanja vya Maisara na kumalizia Hospitali ya rufaa Mnazimmoja.
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 11/03/2020.                                                                        
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja  Dk Ali Salum Ali  amesema juhudi kubwa za utendaji kazi  zinahitajika katika  kuitunza taaluma ya uuguzi ili  kuipatia hadhi kada hiyo nchini.
Aliyasema hayo huko Hospitali ya Mnazi Mmoja katika Sherehe ya Kuadhimisha miaka 200 ya mwasisi wa Uuguzi Duniani.
Amesema kada ya Uunguzi na Ukunga inazidi kuimarika  duniani na kuijengea hadhi hivyo wauguzi wanapaswa kuitunza, kuithamini na kuyatekeleza majukumu yao waliyopangiwa ili kuweza kubadilika kiutendaji.
Dr. Ali aliwataka wauguzi hao kutumia lugha nzuri na kuwa wapole wanapohudumia wagonjwa kufanya hivyo kutasaidia kuwafariji kutokana na hali waliyonayo na kujenga matumaini na sio kutumia lugha chafu ili kuijengea sifa kada hiyo.
Mkurugenzi huyo aliwapongeza wauguzi kwa kutekeleza majukumu yao katika mazingira magumu kwa kufuata utararibu uliowekwa katika kazi zao ili kuhakikisha kuwa wanahudumia kiutendaji.
“Wanastahiki pongezi wauguzi kutokana na kazi kubwa wanayoifanya muuguzi mmoja kuweza kuudumia wagonjwa zaidi ya 34 kutokana na upungufu wa wauguzi”, alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Mkurugenzi huyo aliwasisitiza wauguzi hao kutunza vifaa vya kufanyia kazi zao ili viweze vidumu kwa muda mrefu na kupunguza matatizo ya vitendea kazi, kwani vifaa hivyo vinauzwa kwa gharama kubwa .
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi Zanzibar Bi Amina Abdulkadir aliwataka wauguzi kufanya mabadiliko ambayo yanaweza kuisaidia jamii  kupata maendeleo endelevu  ili kuipa hadhi taaluma hiyo.
“Nasi tunajiamini na tuko juu kiutendaji kwa upande wa Zanzibar taaluma hiyo ilianza mnamo mwaka 1938 hadi sasa inatoa taaluma kuanzia stashahada, shahada ya kwanza na kutarajia hata kuweza kutoa Mastaa’alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt ali Mohamed Shein kwa kuiunga mkono kada hiyo kwa lengo la kuleta mafanikio ya kiutendaji.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Wakunga  Dk. Haji Nyonje Pandu aliiomba Serikali kutoa kipaumbele kwa wauguzi kitaaluma ili iweze kukua zaidi.
Aliwataka wauguzi hao kuwa na mashirikiano ya pamoja katika kuzitatua changamoto zilizopo na kuzifanyia kazi kwa lengo la kufikia malengo kiufanisi.
Alifahamisha kuwa kada ya wauguzi imekuwa soko la ajira duniani hivyo amewataka vijana kusomea katika kada hiyo ili kuondokana na ajira na utegemezi.
Kada ya wauguzi imeanzishwa tarehe 12 mei 1820 huko nchini Londan amabayo imeasisiwa na Mkwe wa Malkia Elizabet.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.