Habari za Punde

Kijue Kirusi cha Corona - Covid-191.    Kirusi hichi hakina uhai lakini ni aina ya protini iliyozungukwa na utandu wa mafuta (lipid fats) ambayo yakipenya kwenye tundu za macho, pua au mdomo hujibadilisha (mutation) na hujizalisha kwa wingi na kuanza kushambulia seli za mwili na hasa mapafu.

2.    Kwa kuwa kirusi chenyewe hakina uhai hakiwezi kuuliwa lakini huharibika wenyewe. Muda wa kuharibika kwake hutegemea na joto, unyevu unyevu na sehemu kilipopatikana.

3.    Kirusi ni kitepetepe mno kwani kimehifadhiwa na utandu mdogo wa mafuta hivyo sabuni yoyote ikitumika kunawia huondosha ule utandu ndiyo maana hutakiwa kuosha mikono kwa kuisugua vizuri kwa uchache sekunde 20 na hapo kirusi huharibika na kutokuwa na madhara tena.

4.    Joto huyeyusha utandu wa mafuta yaliyokizunguka kirusi cha Corona hasa ukitumia maji yenye vuguvugu zaidi ya nyuzi joto 25 kuoshea mikono au hata nguo na chochote chengine.

5.    Aina yoyote ya kilevi chenye zaidi ya asilimia 65, huyeyusha mafuta yoyote hasa ule utandu wa juu wa kirusi cha Corona.

6.    Kirusi cha Corona hakina uhai hivyo hakiwezi kutibika na Antibiotics. Antibiotics hutibu bakteria viumbe walio hai.

Imetafsiriwa kutoka John Hopkins University

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.