Habari za Punde

Kinga Bora Kuliko Tiba Tujikinge na Maambukizo ya Corona Kwa Kunawa Mikono na Sabuni Kwa Maji ya Kutiririka au Kutumia Vitakaso Sanitaiza

Wananchi na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakiingia katika eneo la Wizara hiyo inawalazimu kuosha mikono yao kwa kutumia maji na sabuni ili kujikinga na maambukizo ya maradhi ya virusi vya Corona, kama inavyoonekana picha Tangi la Maji na sabuni likiwa katika eneo hilo.kwa ajili ya matumizi ya kujikinga na Corona.  
Mwananchi akiosha mikono yake kujikinga na maambukizo ya Corona alipokuwa akiingia katika Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar, kama anavyoonekana pichani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.