Mheshimiwa Waziri
Kwanza nitoe shukrani kwa niaba ya Umoja wa Wazalendo na wafanyabiashara
kwako Mhe. Waziri, kwa kuchukua muda wako kujumuika nasi katika shughuli yetu
ya leo ya makabidhiano ya bidhaa , madawa na vifaa vilivyoochangwa au kutolewa
na wafanyabishara, Wazalendo na Marafiki wa Zanzibar
Natambua majukumu makubwa ulionayo ya kitaifa, lakini umeweza
kulipa uzito suala hili. Tunakushukuru sana!
Vile vile ninawashukuru wafanyabiashara, Wazalendo, Marafiki
wa Zanzibar, Taasisi na watumishi wa umma waliojitokeza na kutuunga mkono
katika juhudi zetu za kupambana na mlipuko huu wa virusi vya korona (Covid19 outbreak).
Mheshimiwa Waziri
Ni miezi mitatu
imepita tangu ugonjwa hatari wa korona umeingia duniani. Kasi ya kusambaa kwa
ugonjwa huu inazidi kuongezeka na hatimaye ugonjwa huu umefika nchi nyingi za Afrika
ikiwemo Tanzania. Katika kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein na Serikali yake, Umoja huu wa
Wafanyabiashara na Wazalendo Tanzania Bara na Visiwani haukubaki nyuma katika
mapambano dhidi ya ugonjwa huu, tangu uliporipotiwa duniani na hata
ulipotangazwa kuingia hapa nchini. Tunatambua kuwa, tayari serikali imeweka
mikakati mahususi ya kupambana na ugonjwa huu na kuhakikisha wafanyabiashara na
wananchi wamejiandaa na athari zinazoweza kusababishwa na ugonjwa huu wa
Covid19 kiuchumi, kiafya na kijamii kwa ujumla.
Mheshimiwa Waziri
Kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohammed
Shein na Serikali yake kwenye afya, naomba niwasilishe Architectural Drawings
(Ramani ya mchoro) wa Laboratory Level 3 ambayo kungepenga kuwasilisha kwa
serikali na kama ikiwapendeza serikali, tuje tukae chini kuangalia namna ya
kuisadia Serikali kiujenzi na kwa vifaa
Mheshimiwa Waziri
Umoja huu; umeletamshikamano wa pamoja wa wafanyabiasharana
taasisi mbalimbali za kibishara na umekuwa ukitoa ushirikiano wa karibu kwa
Serikali (Public Private Partnership –
PPP) katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huu yanaleta
ushindi.
Mheshimiwa Waziri
Ushirikiano na moyo wa uzalendo uliopo kati ya umoja huu waWazalendo
na Wafanyabiashara nchini umewezesha kuunganisha nguvu na hatimaye kufanikisha
kupatikana kwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 126 milioni vitakavyosaidia kwenye mapambano
dhidi ya ugonjwa wa corona.
Naomba nitoe orodha ya wale wote waliochangia
Explain the HOTSPOTS areas identified: Malindi Port;Stone Town; Marikiti; Kivingo Beach; Mnazi Mmoja
Hospital; Kiinua Miguu Prison; Soko La Mwanakwerekwe; Bububu; Forodhani Park;
Kituo cha Mabasi Airport; Darajani; Soko la Saateni; Mlandege; Michenzani;
Kariakoo; Rahaleo; Mwembeladu Hospital; Jangombe; Mombasa; Mwera; Ngungwi
Beach; Kiwengwa; etc.
Mheshimiwa Waziri
Umoja wa Wazalendo na ya wafanyabiashara nchini, wakubwa kwa
wadogo wote tumeguswa na tumewiwa kutoa ushirikiano kwa Serikali, jamii na
kwenye maeneo yetu ya kazi kuhakikisha kuwa tunapambana kikamilifu na ugonjwa
hatari wa corona. Napenda tukuhakikishie
Mhe Waziri kuwa Umojahuu wa Wazalendo na Wafanyabiashara nchini utaendelea
kushirikiana na serikali na wadau wengine hadi pale ambapo ugonjwa huu
utakapodhibitiwa kikamilifu.
Mheshimiwa Waziri
Ushiriki wa Umoja huu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa
corona haukwepeki!!. Pamoja na nia njema ya umoja huu, ikumbukwe pia kuwa umoja
huu ambao ndio nguzo ya sekta binafsi una mchango mkubwa katika kujenga uchumi
wa nchi na ndiyo sekta inayozalisha ajira nyingi nchini kwa takribani asilimia
80. Mheshimiwa Waziri, Sekta Binafsi tunashiriki
kwa asilimia mia moja katika mapambano dhidi ya corona kwa kuwa sisi ni sehemu
ya jamii. Tusipofanya hivyo, hakuna atakayebaki salama; na hata biashara zetu
zitakufa pia. Mheshimiwa Waziri, kila
jambo linahitaji watu. Nchi inahitaji watu. Maendeleo yanahitaji watu. Biashara
pia zinahitaji watu, hivyo tuna kila sababu ya kushiriki kujilinda na kuwalinda
wengine,”
Mheshimiwa Waziri
Vile vile Umoja huu unaipongeza Serikali kwa hatua na juhudi makini
ilizochukua hadi sasa. Hatua hizo ni pamoja na kuwahamasisha watanzania
kuchukua tahadhari na kuwa makini wakati wote kwani Kila mtu akitekeleza wajibu
wake wa kujilinda yeye binafsi na kuwalinda wengine tutaweza kuvuka kwa
mafanikio makubwa, hasa ikizingatiwa kuwa walio wengi wanapona hata baada ya kupata
maambukizi ya ugonjwa huu
Mheshimiwa Waziri
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani kubwa
sana kwako, kwa walio hapa na wasiojaaliwa kuwepo ambao wameshiriki kwa hali na
mali nikianzia na:
Mzee wangu Subhash Patel; Motisun and CTI Chairman
Mr Mohammed Bhaloo, Chairman Agha Khan Trust for Culture
Zanzibar
Said Salim Bakhresa (Bakhresa Group)
Dhruv Jog, Advent Construction
Dr. Mohammed Ali, SADC Medical Expert
Abubakar Said Salim Bakhresa
Ambassador Antonio, Brazil (Personal Contribution)
Dr Maryam Lymo, Innovative Projects
Balozi Kindamba
Hamad Hamad,
Zanzibar Chamber of Commerce
Mr. Rahim
Bhaloo, Multi Color Printers Ltd
Parvin
Hasnein
Asha Aslan
Lukman
Fideli Ali
Farid Fazach
Aboud Nassor
Khamis
Nafisa
Jidawi, Wajamama
Zanzibar
Sugar Factory Ltd
Skylink
Travel & Tours
AZAM Marine
Co Ltd
Amsons Group
Camel Oil
Association
of Tanzania Oil & Gas (ATOGS)
ORYX
Energies
Tridea
Cosmetics Ltd
Majid Store
Aruna
Pharmacy
Patel
Import & Export
Bharat
Enterprises
Kay Sotta
Plastic Limited
Print Plus
Mozeti
Virgo Group
Print Plus
Ashton Media
Pamoja na wote waliotoa michango yao ya hali na mali .
Umoja ni nguvu, Utengano ni Udhaifu
Mshikamano Daima!
Asanteni sana
Imetolewa na
Hon. Abdulsamad Abdulrahim
On
Behalf of the entire Business Community, Patriotism and Friends of Zanzibar
both in Mainland Tanzania and Zanzibar
Telephone: 0779 060 338
Email: a.abdulrahim@atogs.or.tz
No comments:
Post a Comment