Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Atembelea Bohari Kuu la Madawa Maruhubi Jijini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati wa ziara yake Bohari Kuu ya Madawa Zanzibar na kuuagazia Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kukaa pamoja na Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar ili kupanga namna bora ya kufikisha huduma nzuri kwa wagonjwa waliopo katika vituo mbali mbali ikiwemo huduma nzuri ya Chakula.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Mfanyakazi wa Bohari Kuu ya Madawa Zanzibar wakati wa ziara yake, akitowa maelezo jinsi ya upangaji wa dawa na usimamizi wa kuzisambaza katika Hospotali na Vituo vya Afya Zanzibar.    
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed wakitembelea Bohari Kuu la Madawa Maruhubi Jijini Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Bohari hilo leo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi  akiwa na moja ya dawa zinazohifadhiwa katika Bohari hilo wakati akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Zanzibar.Ndg.Zaharan Ali Hamad, akiwa katika ziara yake leo kutembelea Bohari Kuu la Dawa Maruhubi Jijini Zanzibar.
Na,Kassim Abdi.OMPR.
Uongozi wa wizara ya Afya umetakiwa kuweka utaratibu wa  kuwapitia                        mara kwa mara wagonjwa wa Corona kwenye vituo vilivyoanzishwa pamoja na watu              waliowekwa katika karantini ili kuelewa changamoto zinazowakabili wagonjwa waliopo    kwenye vitu hivyo na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi kwa wakati changamoto hizo.       
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif ali Iddi ameeleza hayo wakati alipotembelea Bohari 
kuu ya dawa iliopo Maruhubi ili kujionea mwenyewe uhifadhi wa dawa na vifaa vyengine vya kupambana na  maambukizi ya maradhi ya corona.
Balozi Seif alisema wagonjwa pamoja na watu waliopo kwenye karantini wanapaswa kupatiwa huduma nzuri ikiwemo chakula bora ili kuzifanya Afya zao kuimarika 
kwa haraka na kurejea katika harakati zao za maisha. 
“Miongoni mwa mambo yanayosababisha  kutengemaa afya ya mgonjwa  ni pamoja na 
kupata chakula bora na kwa wakati’’ Alisistiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif  alitumia fursa hiyo kwa  kuwapongeza wafanyakazi,  
madaktari, waaguzi na watoa huduma wote kutoka wizara ya Afya kwa moyo wao wa kujitolea katika kuwahudumia wagonjwa na kuwaahidi kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Aidha, Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya kukaa pamoja na Kamisheni 
ya kukabiliana na Maafa kwa lengo la kujadili utaratibu mzuri utakaotumika katika kulipati
a ufumbuzi suala la upatikanaji wa chakula kizuri kwa wagongwa waliopo katika vituo mbali mbali.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Hamadi Rashid Mohamed alimueleza Makamu wa Pili wa Rais  kuwa wizara yake inaendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa maambukizi ya Covid 19 kupitia kikosi kazi  chake huku wizara ikiwa na mpango wa kuwapatia mafunzo madaktari wengine ili kuongeza nguvu katika kutoa huduma. 
Mhe. Hamadi alifafanua kuwa Wizara ya Afya inachukua jitihada kubwa katika kuwafuatilia 
watu waliotajwa kukutana na wahusika wanaoshakiwa kuambikizwa virusi vya Coron
a hali ambayo imepelekea shirika la Afya duniani WHO kuiopongeza Zanzibar juu ya 
hatua wanazozichukua katika kakabiliana na maradhi hayo.
Pia, Waziri huyo aliwasisitiza wananchi kuchukua jitihada za maksudi ili kujilinda 
mtu binafsi na famili yake kwani kufanya hivyo kutapelekea kupunguza kasi ya 
kusambaa ya maradhi hayo.
Nae Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Ndugu Zahrani Ali Hamad alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kwamba vifaa vilivyopo sasa ambavyo vyengine vimetolewa msaada kwa ajili ya kuwafikia wagonjwa watahakikisha vinatumika kama ilivyokusudiwa huku kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kuendelea kuvigawanya vifaa hivyo katika vituo mbali mbali vya Unguja na Pemba.
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa wafanyakazi waliopo katika Bohari hiyo wanafanya kazi ya kugawa dawa pamoja na kuzisambaza katika vituo husika kwa mujibu wa maombi yalivyowafikia.
Vifaa vilivyopo katika Bohari hiyo ni pamoja vitakasa mikono, nguo maalum kwa ajili watoa huduma kwa wagonjwa, na maji na vifaa vyengine kwa ajili ya kujikinga na Corona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.