Habari za Punde

Migahawa Yafunguliwa Kenya Huku Watu 8 Zaidi Wakiambukizwa Virusi Vya corona.

Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe ametangaza watu wanane zaidi wameambukizwa virusi vya corona nchini humo na pia kulegeza masharti kwenye migahawa inayouza chakula.
Tangu mara ya kwanza kutangazwa kwa virusi hivyo, idadi jumla ya walioambukizwa nchini Kenya imefikia 363.
Aidha 8 pia wamethibitishwa kupona na kufikisha jumla ya idadi hiyo kuwa 114.
Wote walioambukizwa hawana historia ya kusafiri ya nje ya nchi hali inayoashiri kwamba bado kungali kuna maambukizi ya ndani kwa ndani nchini humo.
Wizara ya afya pia imesema kuwa itaruhusu migahawa kuanza kufunguliwa kuanzia saa 11 asubuhi na 10 jioni.
Watakaoingia kuhudumiwa watahitajika kufuata utaratibu uliopo wa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa kama kawaida. Hatua ya kutokaribiana itaendelea kutekelezwa umbali wa mita 1 baina ya mtu mmoja hadi mwengine.
Lakini watakaoruhusiwa kutoa huduma ni wale watakaokuwa wamepimwa pekee.
Pia kulingana na wizara ya afya, katika migahawa hiyo, huduma ya kujiwekea chakula bado imesitishwa.
Wizara hiyo imetoa agizo la watu wote wanaoingia migahawani kupimwa kiwango cha joto na kuruhusiwa tu kuingia ikiwa litakuwa chini ya nyuzi 37.5 na mgahawa husika kuarifu wizara mara moja kuhusu mtu atakayepatikana akiwa na kiwango ha juu zaidi ya hicho, kwa kupiga simu kupitia nambari 719 ili kupata mwongozo zaidi.
Bwana Kagwe amewataka raia wote wa Kenya kuendeleza nidhamu na kuchukua jukumu wao wenyewe binafsi katika juhudi za kubabiliana na janga hili.
"Hali ya Kenya itabadilika kwasababu yako wewe. Ikiwa tutajuchukua jukumu kama watu binafsi, bila shaka tutakabiliana na virusi hivi," Kagwe amesema.
Waziri pia amegusia kwamba sasa Wakenya wameanza kutekeleza sheria na kanuni zilizowekwa na serikali upande wa usafi.
"Visa vya matatizo ya tumbo vimepungua tena pakubwa, visa vya kuharisha vimepunga," waziri kagwe amesema.
Katika kukabiliana na ugonjwa wa covid-19, serikali imeunda kamati 5 za kimkakati kutoa mwongozi wa njia zitakazofanikisha kenya kushinda vita hii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.