Habari za Punde

UNUNUZI TIKETI MITANDAONI KUDHIBITI CORONAKATIKA kukabiliana na mambukizi ya virusi vya Corona katika vituo vya mabasi serikali
imesema mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao utaanza hivi karibuni kwa mabasi
yote yanayofanya safari zake mikoani.

Mbali na mabasi hayo, daladala pamoja na mabasi ya mwendokasi yanatarajiwa (Data
center) ambapo mfumo huo utarahisisha huduma na kuondoa adha ya wapiga debe vituoni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ,
Mhandishi Isack Kamwele, wakati wa ukaguzi wa mifumo hiyo jana Dar es Salaam alisema
hatua hiyo itafikiwa hivi karibuni ambapo kiu ya serikali ni kuona wananchi wananufaika kwa kuondoshewa adha ya usafiri.

Mhandisi Kamwelwe alisema serikali imefikia hatua ya mwisho ya kuanza kutumika kwa
mfumo huo ambapo wananchi watatumia simu kukata tiketi za mabasi na hawatolazimika
kutembelea vituoni jambo litakalowaepusha na wizi unaofanywa kupitia ulanguzi wa tiketi
na wapiga debe.

“Nimeridhishwa na mfumo, huu ambao utasimamiwa na serikali kupitia kituo chetu cha
Data center ukweli utasaidia sana wananchi wetu hususani wale wa chini ambao walikuwa
wanaingia gharama kwenda katika vituoni kukata tiketi, tumefika wakati wa kuwa kisasa
zaidi wapiga debe walikuwa wakiongeza gharama lakini wakati huu wa maambukizi ya
corona ni muhimu kutafuta njia mbadala katika usafirishaji,”alisema.

Mhandisi Kamwele alisema, mfumo huo ameungahikia kwa muda mrefu hatimaye sasa
unafika mwisho ambapo ameridhaka na uandaaji wa kimifumo kwakuwa taarifa zitatunzwa
vizuri na kufanya kazi kwa ushirikishi wa wadau wa usafiri nchini.

“Hakuna sababu ya msafiri kutembea na pesa mkononi, hata wanaopandia njiani ni wakati
wa kuwa na pesa kwenye simu, kwakuwa hatuna uhakika iwapo ugonjwa huu utaeneo hadi
kwenye noti ni lazima kuwa na njia nyingi za udhibiti,”alisema

Alisema wamiliki wa mabasi walikuwa na maswali mengi wakati wa mchakato wa mfumo
huo, wakihofia kupata hasara lakini ni wazi utendaji wake utanufaisha pande zote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.