Habari za Punde

Vijana watakiwa kuwa wazalendo ili kuijenga nchi yao

Zanzibar.                                                            26-04-2020.
Vijana wametakiwa kuisoma Historia ya Zanzibar ili wapate Uzalendo wa kuilinda na kuipenda nchi yao.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais Ahmada Yahya Abdul-wakili wakati alipokuwa akizungumza na Zbc kuhusiana na miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema baadhi ya Wanasiasa wanawapotosha Wananchi kwa kuwapa Historia isiofaa  jambo ambalo linawafanya Vijana kukata tama na kufanya mambo kinyume na Maadili ya nchi.
Aidha amesema hali ya Uzalendo wa Vijana katika kujitolea  imepunguwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Vijana wa zamani  hivyo ni vyema kufanya kazi kwa kujitolea zaidi ili kuzidi kuimarisha na kudumisha Muungano huo.
Mbali na hayo amesema tokea kuasisiwa kwa Muungano huo,Zanzibar imeweza kufaidika katika mambo mbalimbali ikiwemo Ulinzi na Usalama na elimu ya juu jambo ambalo linapaswa kuendelezwa kwa faida ya sasa na kuzazi kijacho.
Hata hivyo amewaomba Wananchi kuendelea kudumisha Amani na utulivu iliopo ili waweze kujipatia maendeleo katika Nyanja mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.