Habari za Punde

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi afikisha miaka 95

HAPPY BIRTHDAY

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei 1925) alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia 1985 hadi 1995.

Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa.

Pia, Mwinyi alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.

Mzee Mwinyi aliwahi pia kuwa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Wakati wa utawala wake wa mihula miwili, Mwinyi alichukuwa hatua za mwanzo kubadilisha sera za ujamaa za Mwalimu Nyerere. Alilegeza vikwazo vya manunuzi ya nje na kuhamasisha watu kuanzisha biashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.