Habari za Punde

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KUMI NA TISA WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2020/2021 UTAKAOANZA KESHO JUMATANO TAREHE 6 MEI, 2020.


Ndugu Waandishi wa Habari na wananchi kwa ujumla, Mkutano wa Kumi na Tisa  wa Baraza la Tisa la Wawakilishi unatarajiwa kuanza kesho Jumatano  ya tarehe 06 Mei, 2020, saa 3:00 asubuhi.
Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

1.   Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2020/2021.


2.   Miswada ya Sheria

Miswada miwili ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa, Miswada yenyewe ni:-

i)     Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)

ii)   Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2020/2021.

  
Ratiba ya  Awali ya ya Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-
TAREHE
TUKIO/WIZARA
06/05/2020  -  07/05/2020
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
07/05/2020  -  08/05/2020
Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
11/05/2020  -  12/05/2020
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ
13/05/2020  -  14/05/2020
Ofisi ya Rais  Utumishi wa Umma na Utawala Bora
14/05/2020 -  15/05/2020
Wizara ya Katiba na Sheria
18/05/2020  -  19/05/2020
Wizara ya Habari, Utalii, na Mambo ya Kale
19/05/2020  -  20/05/2020
Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto
21/05/2020  -  22/05/2020
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
25/05/2020   - 26/05/2020
Sikukuu ya Eid el Fitri
27/05/2020  -  28/05/2020
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
28/05/2020  -  29/06/2020
Wizara ya Biashara na Viwanda
01/06/2020  -  02/06/2020
Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo
02/06/2020 -   03/06/2020
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
04/06/2020  -  05/06/2020
Wizara ya Afya
08/06/2020  -  09/06/2020
Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati
09/06/2020  -  10/06/2020
Wizara ya Fedha na Mipango
11/06/2020  -  12/06/2020
Majumuisho ya Mijadala ya Bajeti za Wizara zote baina ya Serikali na Kamati ya Bajeti
15/06/2020 Saa 3.00 Asubuhi
Hotuba ya Mpango wa Maendeleo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2020/2021
Saa 5.00 Asubuhi

Hotuba ya Kamati ya Bajeti Kuhusu Majumuisho ya Mjadala ya Bajeti za Wizara za SMZ
Saa 6.00 Mchana
Hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2020/2021
16/06/2020, 17/06/2020  -  18/06/2020
Mjadala wa Hotuba ya Mpango wa Maendeleo wa SMZ 2020/2021 na Hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2020/2021
19/06/2020 
Mswada wa Sheria ya Matumizi (Appropriation Bill)
Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)

Hata  hivyo , Mazingira ya majadiliano ndani ya Baraza yanaweza kuifanya Ratiba hii isifuatwe kwa ukamilifu. 
TANBIHI 
Ndugu Wananchi/ Waandishi wa Habari
Kama tunavyofahamu , Mkutano huu unafanyika wakati ambao nchi yetu na ulimwengu kwa ujumla tupo katika janga kubwa la ugonjwa wa CORONA.  Hivyo, katika kuendesha Mkutano huu kwa mazingira yaliyopo, Baraza la Wawakilishi linaendelea kuchukua tahadhari mbali mbali kwa kutambua umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya maradhi ya CORONA.
Miongoni mwa hatua ambazo Baraza la  Wawakilishi linaendelea kuchukua ni pamoja na zifuatazo :-
a)   Kupunguza  Muda wa Vikao
b)   Kurekebisha ukaaji wa Wajumbe kwa kuacha nafasi kuanzia  mita Moja baina ya Mjumbe na Mjumbe
c)    Kuweka Vifaa   vya kuoshea Mikono katika Maeneo yote ya Baraza
d)   Kuweka Vifaa vya kupima joto na kuwapima Waheshimiwa Wajumbe na Wafanyakazi  na maafisa wote  watakaohudhuria katika vikao hivyo.
e)    Kuruhusu maafisa wachache sana kutoka  Mawizarani watakaohusika moja kwa moja na hoja inayojadiliwa
f)     Hakutakuwana wageni ikiwemo wanafunzi au wananchi wanaotembelea Baraza kwa ajili ya kuangalia shughuli za Baraza au kujifunza.
g)    Kutoruhusi mtu yeyote kukaa katika mazingira ya nje ya ofisi za Baraza.
Ahsante.

(Raya Issa Msellem)
KATIBU
BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR
Mei 5 , 2020


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.