Habari za Punde

Taasisi ya One Ummah Yakabidhi Vyakula Kwa Wananchi.

Na.Takdir Suweid Maelezo Zanzibar.
Jumla ya sh.milioni mia moja na ishirini zimetumika kwa ajili ya vyakula mbalimbali kama Tende,Mchele na Sukari katika kaya 1000 Masikini za Unguja na Pemba,zilizotolewa na Taasisi ya Ummah Ofisi ya Zanzibar.
Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi wa Taasisi ya One Ummah Ali Haji Ali amesema vyakula hivyo vimezingatia Wananchi wa Kaya masikini zaidi.
Aidha ameahidi kuwa Taasisi yake itaendelea kutoa msaada zaidi ya hali na mali kwa Watu hao kadri hali itakaporuhusu.
Aidha amesema lengo ni kusaidia Wananchi wa Zanzibar katika Nyanja mbalimbali kama vile kuchimba visima,kujenga Miskiti,kujenga Madrasa,kuftarisha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kurudisha udugu,upendo na ushirikiano kwa jamii.
Hata hivyo Mkurugenzi Ali amesema tatizo kubwa linalowakabili ni Miradi midogo ukilinganishwa na mahitaji ya Wananchi hivyo amewaomba Wafadhili wa Taasisi mbali mbali kushirikiana katika kuwasaidia Wananchi wenzao katika maeneo mbalimbali.
Nao baadhi ya Wanakaya masikini waliopatiwa msaada huo katika vijiji vya Bumbini,Bwejuu,Bambi na kisiwa cha Kokota Pemba wameishukuru Taasisi ya One Ummah kuwapa msaada huo na kuomba Watu wengine kuwasaidia kwa hali na mali katika kupambana na hali ngumu ya Maisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.