Habari za Punde

RC Kusini Pemba akagua uvaaji wa barakoa Chakechake

 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akitoa maelekezo kwa kondakta wa gari ya abiria ruti Chake - Pujini, baada ya kupakia abiria ambao hawakuvaa Barakoa na kutakiwa kwenda kuwanunulia, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na vijana ambao waliokuwa wamepanda kwenye Toni Haisi bila ya kuvaa barakoa, huku akiwataka vijana hao kutokupanda gari bila ya kuvaa barakoa, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)


MMOJA ya abiria aliyeshushwa katika gari aina ya Toni Haisi katika eneo la ukaguzi wa barakoa Chanjaani, akinunua barakoa yake katika moja ya maduka yaliyopo chanjaani kama alivyokutwa na kamera ya Zanzibar leo, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla,. akizungumza na wanafanya biashara wa nguo za mitumba katika soko la jumapilia Chake Chake, kuhakikisha wanapunguza msongomano wa wananchi wanaochagua nguo hizo, pamoja na kuvaa barakoa kwa wauzaji na wanunuzi, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na wanafanya biashara wa soko la matunda na mboga mbonga juu katika mji wa chake chake, juu ya uvaaji wa barakoa na kuwapongeza wafanya biashara hao, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 BAADHI ya wananchi wa Chake Chake, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, juu ya ushajihishaji wananchi kuvaa barakoa, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akimtaka mmoja ya wafanya biashara wa mihogo katika soko la Tibirinzi, kuacha uchewe wa kuvaa mfuko badala yake kutafuta barakoa kuvaa, wakati wa zoezi la msako kwa wananchi wasio vaa barakoa katika mji wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.