Habari za Punde

Wafadhili waombwa kuwasaidia wenye ulemavu kuweza kujikimu

Na Takdir Suweid
Wafadhili na Watu wenye uwezo wameshauriwa kusaidia misaada mbalimbali kwa makundi maalum ikiwemo Watu wenye Ulemavu ili waweze kujikimu katika kipindi cha Janga la Corona na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Ushauri huo umetolewa na Mwanaharakati wa masuala ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Nuru Ali Ussi wakati alipokuwa akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari huko Mombasa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’.
Amesema Makundi hayo yanakabiliwa na ugumu wa maisha hivyo yanahitaji kusaidiwa Vyakula, Nguo na Vifaa vya kujikinga na Corona ili kupungua ukali wa maisha.
Aidha ameziomba Taasisi Binafsi,Viongozi wa vyama vya Siasa, Mikoa, Wilaya na Majimbo kuzidi kuyapa kipao mbele makundi hayo wakati wanapopanga Mikakati ya kimaendeleo na kutoa Misaada kwa Wananchi wao.
Hata hivyo amewaomba Wazazi wa Watoto wenye ulemavu kuacha kuwafungia majumbani kwani kufanya hivyo ni kuenda kinyume na Sheria za nchi na Mikataba ya kitaifa ya haki za Binadamu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.