Habari za Punde

Makada wa CCM warudisha Fomu za kugombea uchaguzi kupitia CCM . Bhaa ajiondoa

 KADA wa Chama cha Mapinduzi CCM, Perira Ame Silima, (kulia) akirudisha fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar, kwa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni Zanzibar, Galos Nyimbo, baada ya kukamilisha zoezi zima la ujazaji wa fomu hizo.
 MWANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bakari Rashid Bakari, (kulia) akikabidhi fomu za wadhamini kwa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni Zanzibar, Galos Nyimbo, baada ya kukamilisha zoezi zima la ujazaji wa fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais kupitia Chama cha CCM.
  MWANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi CCM, Hasna Masoud Attai, (kulia) akirudisha fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar, kwa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni Zanzibar, Galos Nyimbo, baada ya kukamilisha zoezi ujazaji wa fomu hizo.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Mtoni na Mbunge kupitia CCM, Ibrahim Hussein Makungu, akionesha fomu zake  baada ya  kujiondoa katika kinyanganyiro cha  kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar kupitia Chama cha CCM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.