Na
Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augistino Lyatonga Mrema
akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu kumuunga mkono Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani mwaka huu 2020.
Mwandishi Wetu, MAELEZO, DAR ES SALAAM 24.6.2020
MWENYEKITI wa Chama cha
Tanzania Labour Party, Augustino Mrema amesema chama hicho kinaendelea na
msimamo wake wa kumuunga mkono, Rais Dkt. John Magufuli kuwa mgombea wake wa
nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa
kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi
wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho,
Augustino Mrema alisema kuwa katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
Serikali ya Awamu ya Tano imekilazimu chama hicho kuunga mkono kuwa TLP
haitosimamisha mgombea na badala yake Rais Dkt.John Magufuli apitishwe kuwa
Mgombea wa Kiti cha Urais wa Tanzania mwaka huu kwa hoja kuu tano.
“Tanathamini Kazi
zinazofanywa na Mhe. Dkt John Magufuli na
asilimia 98% ya wajumbe kwenye Kamati Kuu na 100%
kwenye Halmashauri Kuu walitoa pendekezo la TLP kutoweka mgombea wa Urais na
badala yake chama kimuunge Mkono Mgombea wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mh Dk
John Pombe Joseph Magufuli” alisema Mrema
Alisema kuwa katika
kutekeleza kazi za maendeleo Uongozi wa Rais Dkt John Pomnbe Magufuli
ulishughulikia suala la Watumishi hewa kuwaondoa watumishi wenye dosari wapatao 32,555
sawa na asilimia 5% ya watumishi wote Serikalini na kuokoa pesa Tshs 19.8bln
kwa kila mwezi sawaTshs 237.6 bln kwa mwaka.
Alibainisha suala lingine
linalofanya TLP kumuunga mkono Dkt John Magufuli ni kuhusu kusambaza umeme wa
uhakika mjini na vijiji kitu ambacho siku za nyuma kidogo hakikuwezekana lakini
katika utawala wake umeme umefika hadi vijijini
“Wakati Mhe Dk John Pombe
Joseph Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 palikuwa na vijijini 2,018 tu
vyenye umeme kwa lugha rahisi tangu Tanzania ipate uhuru ni vijiji 2,018 tu
kati ya vijiji 12,268 sawa 17% ndio vilikuwa na lakini mpaka sasa vijiji 9,112
sawa na asilimia 74.3, ambalo ni ongezeko la vijiji 7,094 sawa na asilimia
57.3”, alibainisha Mrema.
Aliongeza kuwa katika
sekta ya ujenzi wa Miundombinu Serikali ya Dkt.John Magufuli imejikita katika
kubadilisha mandhari ya Tanzania katika Majiji, Miji na vijiji mabili
mbali.
Alisema kwa upande wa
miradi, Tanzania imeendelea kufanya vizuri, huku akitolea akilitaja jarida la The Africa Construction trend report 2019”
linaloonyesha jumla ya miradi 51 ya Tanzania ikiwa na thamani ya thamani ya
Dola za Marekani Bilioni 60.3 ya thamani ya miradi yote.
No comments:
Post a Comment