Habari za Punde

Viongozi na Wafadhili Kushirikiana na Halmashauri Kulitafutia Ufunmbuzi Tatizo la Njia za Ndani.

Na.Takdir Suweid Zanzibar
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘’A’’ Ndg. Mussa Ali Makame amewashauri Viongozi na Wafadhili kushirikiana na Halmashauri yake katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la ubovu wa njia za ndani ili kuwaondoshea usumbufu Wananchi.
Amesema iwapo Wabunge, Wawakilishi, Madiwani na Wafadhili watashirikiana na na Halmashauri hiyo,tatizo la ubovu wa ndani litaweza kuondoka kwa kuzifanyia matengezezo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari huko Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini ‘’A’’ amesema katika Halmashauri hiyo kuna njia zaidi ya 20 zinazohitaji kufanyiwa matengenezo lakini bajeti yao haijarishisha.
Hivyo amewashauri Wafanyabiashara,Wamiliki wa Hoteli na Taasisi nyengine zilizomo katika Halmashauri hiyo kulipa Kodi za Halmashauri ili ziweze wapate mapato ya kuzifanyia ukarabati njia hizo.
Hata hivyo amewakumbusha Viongozi wa Wadi na Shehia kuibua kero za Wananchi na kuzipeleka sehemu husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka na kuondosha kero kwa Wananchi wao wanaowaongoza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.