Balozi Joseph Sokoine
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akisalimiana na Bi. Christine Musisi
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada
ya mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba - Dodoma.
Pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili namna ya kuimarisha ushirikiano
katika masuala ya mazingira
Balozi Joseph Sokoine Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) akiwa katika kikao pamoja na ujumbe
kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine
Musisi ambae ni Mwakilishi Mkazi. Kikao
hicho kimelenga kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya Mazingira hususan
katika maeneo ya Mabadiliko ya Tabianchi, Uchumi wa Bahari, Nishati endelevu, Hifadhi
ya Bioanuai na Ikolojia. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais
Mtumba - Dodoma.
Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi - Mwakilishi Mkazi
mara baada ya kukamilika kwa kikao cha mashirikiano baina yao. Wengine katika
picha ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na UNDP.
Balozi Joseph Sokoine Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiagana na Bi. Christine Musisi Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya kukamilika
kwa mkutano baina yao uliojadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika masuala
ya mazingira. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba –
Dodoma.
No comments:
Post a Comment