Habari za Punde

Mapokezi Makubwa ya Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi Akiwasili Zanzibar Akitokea Dodoma leo.

Mgombea Urais wa Zanzibar  kupitia Chama cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono Wananchi wa Zanzibar katika eneo la michezani Jijini Zanzibar, wakati wa mapokezi yake akitokea Dodoma, akielekea Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika gari maalum ilioandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake alipowasili Zanzibar akitokea Dodoma leo.
Bendi ya Vijana wa UVCCM Chipukizi wakiongoza msafara wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Cha Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi wakielekea Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar kwa ajili ya mapokezi na kuzungumza na Wanachama wa CCM Zanzibar.
Wananchi wa Zanzibar wajitokeza katika mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika eneo la michezani Jijini Zanzibar.
Wapanda Pikipiki Zanzibar wakiwa katika msafara wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Cha Cha Mapinduzi wakielekea katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Wapanda Pikipiki Zanzibar wakiwa katika msafara wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Cha Cha Mapinduzi wakielekea katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Cha Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, akifungwa kiskafu na Kijana wa Chipukizi Zaadia Mbarak, baada ya kuwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, akitokea Dodoma baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa CCM. 
MGOMBEA Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya Viongozi wakiitikia dua wakimuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kaburi leke lililoko katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Mgombea) Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na (kulia kwa Mgombea) Makamu wa Pili wa Rais wa Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid wakiitikia dua
Wake wa Viongozi wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. wakati wa hafla ya mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.