Habari za Punde

TANTRADE YAISHUKURU NBC KWA KUWADHAMINI WAJASIRIAMALI KATUKA MAONESHO YA 44 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2020

Mamlaka ya Uendelezaji Biashara na Masoko Tanzania (TanTrade) imeishukuru benki ya NBC kwa kuwawezesha wajasiriamali kushiriki maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam mwaka huu wa 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa TanTrade  Bi Latifa Khamis wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye viwanja vya Julius Nyerere, maarufu sabasaba ili kutoa shukran kufuatia udhamini huo.

“NBC ni miongoni mwa taasisi ambazo zimekuwa zikituunga mkono kwa takriban miaka minne mfululizo, ni wadau wakubwa wa maonesho haya ya sabasaba, kupitia udhamini wao wa shilingi milioni 80 wamewawezesha wajasiriamali kushiriki maonesho haya wakiwa na bidhaa zenye viwango vinavyohitajika bidhaa zao ziko kwenye standards za kimataifa.” Alisema.

Kwa upande wake, Bw. William Kalaghe aliwapongeza Tantrade kwa kuwezesha maonesho kufanyika katika kipindi kifupi na ndio maana NBC iliamua kuwa sehemu ya taasisi zilizounga mkono maonesho haya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.