Habari za Punde

Wataalamu wa Afya watakiwa kushirikiana kuwasimamia wahudumu wa afya wa kujitolea

 Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk Fadhil Mohamed Abdalla akizungumza katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za smz, Khalid Abdalla Omar akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.


 Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko Sekta ya Afya Subira Suleiman Khatib akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi katika Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.

 Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za smz akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi na washiriki wa Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
 Msaidizi Meneja Program Shirikishi Ukimwi,Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya Issa Abeid Mussa akitoa mada katika Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.

 Msaidizi Mkuu Kitengo cha Elimu ya Afya Abdurahman Kwaza akiwasilisha mada katika Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Halima Ali Khamis akitoa mada ya Jamii ni Afya katika Mkutano kuhusiana na Mkakati wa Uwasilishaji wa Mkakati wa Afya ya Jamii uliofanyika katika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Maelezo Zanzibar       28/07/2020
 Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  anaeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Khalid Abdalla Omar amewataka wataalam wa Afya kushirikiana na kuwasimamia wahudumu wa afya wa kujitolea ili kutekeleza vyema majukumu yao.
Naibu katibu huyo ameyasema hayo huko Hotel ya Verde katika hafla ya ufunguzi wa Uwasilishwaji wa Mkakati wa afya ya jamii.
Amesema wahudumu wa afya wa kujitolea wana mipaka yao katika utekelezaji wa kazi zao hivyo ni vyema kuhakikisha kwamba wanasimamiwa ipasavyo  katika kufanikisha majukumu yao
Amefahamisha kwamba sio vizuri kuachiwa kufanya majukumu yasiyowahusu ili kujiepusha kupata madhara kwa jamii.
“Wahudumu wa afya wa kujitolea wana mipaka yao katika utekelezaji wa kazi zao naomba sana tuwasimamie kutekeleza majukumu yao bila ya kukiuka mipaka ya kuwatumia kufanya majukumu ya wataalam wa afya”, amesisitiza Naibu Katibu huyo.
Naibu huyo ameeleza kuwa iwapo watawatumia ipasavyo wahudumu hao watasaidia kuimarika huduma za afya kwa jamii pamoja na kufikisha huduma hiyo kwa ukaribu.
“Tukiwatumia ipasavyo tutakuwa tumeifikia jamii kwa karibu sana na hilo litapelekea afya za Wazanzibar kuimarika”, alieleza.
Mapema Mkurugenzi Kinga kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja Fadhil Mohamed Abdalla amewasisitiza wahudumu hao kufuata sheria na kanuni za Mkakati huo kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma ya jamii na kupata taifa lenye vijana imara.
Nao washiriki hao wamepongeza kuanzishwa mkakati huo na kuahidi kutekeleza vyema majukumu yaliweka ili kuweza kutoa huduma bora na kuzidi ubora wa uimarishaji wa huduma hiyo kwa jamii   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.