Habari za Punde

Kamati Kuu ya CCM Imezipomgeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduziu Zanzibar.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika Mkoani Dodoma leo,19,Agosti 2020, ( kulia kwa Mwenyekiti) Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kilichokaa leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kimezipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa yaliopatikana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein naye alihudhuria katika kikao hicho ambacho kimefanyika leo mjini Dodoma.

Katika taarifa ya Umma kuhusu kikao cha Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole ilieleza kuwa miongoni mwa mafanikio hayo ni utekelezaji mzuri wa Dira ya Taifa ya mwaka 2020/2025, Mwelekeo wa Sera za CCM kwa miaka ya 2010-2020, Ilani ya CCM ya 2015-2020 pamoja na usimamizi madhubuti wa Sera za kiuchumi nchini.

Kufuatia mafanikio hayo kwa kauli moja Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar kwa mafanikio hayo makubwa yaliopatikana.

Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilikaa leo kikiwa na lengo la kuandaa agenda ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Kwa maelezo ya Polepole Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itakutana kesho tarehe 20 Agosti 2020 katika Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma.

Sambamba na hayo, taarifa hiyo ilieleza kwamba pamoja na kujali na kupitisha agenda za Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa Kikao hicho cha Kamati Kuu kinakuwa cha kwanza baada ya Tanzania kuvuka na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa Kati.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.