Habari za Punde

Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Dr. Hussein Mwinyi Amechukua Fomu leo Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji Mkuu Mstaaf Mhe. Hamid Mahmoud Hamid, akimkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dr.Hussein Ali Hassan Mwinyi, alipofika leo Ofisi za Tume Maisara kuchukua fomu ya Uteuzi wa Mgombea Urais wa Zanzibar. hafla hiyo imefanyika leo 26/8/2020, akiwa mgombea wa kwanza kuchukua Fomu ya Urais leo asubuhi.
Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wandishi wa Habari mara baada ya kuchukua Fomu  ya Uteuzi wa Mgombea wa nafasi hio katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Maisara Zanzibar.




Mwashungi Tahir   Maelezo 26-8-2020.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema hatowafumbia macho wabadhirifu watakaohujumu wa mali za Serikali.
Ameyasema hayo huko katika ofisi ya Kisiwandui wakati alipokuwa akizungumza na wanacama wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuchukuwa fomu ya Urais ambapo uchaguzi unatarajiwa kutafanyika Oktoba 2020.
Amesema mara atakaposhika nafasi ya Urais  atahakikisha anadhibiti ubadhirifu wa mali ya umma ikiwemo rushwa, wahujumu wa uchumi na wale wasioitakia nchi mema .
Aidha amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi wawe mstari wa mbele  kuilinda amani iliopo ili nchi iendelee kuwa na  utulivu.
“ Wanachama wenzangu tujitahidi kuilinda amani  iliopo nchini  kwani bila amani hakuna maendeleo”, alisema Mgombea huyo.
Pia ameahidi ataiendeleza miradi yote iliyokuwa ameianzisha DKT Shein ambayo hakuwahi  kuimaliza na kutumika kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo amesema ataimarisha viwanda ili  vijana waweza kupata ajira na kuboresha  sehemu za utalii, bandari na uvuvi ili uchumi uweze kukua.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdullah Juma Mabodi amewataka wanachama chama cha  Mapinduzi   kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura ili ushindi upatikane kwa kishindo.
Kwa upande wa wanachama wa chama cha Mapinduzi wameahidi wataitumia haki yao ya msingi ifikapo muda wa kupiga kura na kuhakikisha CCM inashika dola  kwa mara nyengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.