Habari za Punde

Vikundi vya Usafi Zanzibar Washiriki Katika Kufanya Usafi Maeneo ya Mbweni Matreka Jijini Zanzibar.

Baadhi ya Washiriki katika zoezi la  Safisha Zanzibar wakifanya usafi katika eneo la mbweni matreka wakifanya usafi katika eneo hilo,  Baadhi ya washiriki katika zoezi la safisha Zanzibar wakiwa katika harakati za usafishaji huko Matrekta Mbweni Jijini Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika eneo la mbweni lililoandaliwa na Jumuiya ya Safisha Zanzibar ,Wajimama na Baraza la Manispa Wilaya ya Magharibi " B"  hafla hiyo imefanika katika maeneo ya mbweni.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa katika matayarisho ya kuchangia damu kwa hiari zoezi lililofanyika Mbweni Matrekta mara baada ya kumaliza kufanya usafishaji katika eneo la mbweni Matreka.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo yakale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari juu ya suala zima la umuhimu wa  usafi huko Mbweni Mjini Zanzibar.
Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar.

Na.Mwashungi Tahir   Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kupatiwa elimu kwa lengo la kuwa na utaratibu wa kuweka  usafi katika mazingira wanayoishi.
Wito huo ameutoa huko Mbweni wakati alipokuwa akizungumza na vikundi vya usafishaji vya WAJAMAMA ambayo ni kampuni inayoweka akinamama na watoto katika hali ya usafi na kuwa na afya bora  wakishirikiana  na Safisha Zanzibar  kwa lengo la kuona mji unakuwa safi na unavutia .
Amesema jamii inaona labda usafi ni wa Serikali peke yake au manispaa  dhana hiyo indoshwe kwani kila binaadamu au kiumbe chochote kinahitaji kuwa na mazingira ya usafi sehemu anayoishi hivyo jitihada za kutoa elimu zinahitajika zaidi.
Hata hivyo amesema iwapo usafi utakuwemo nchini maradhi ya mripuko hayataweza kutokea Bajeti ya dawa itapungua  uchumi utaongezeka    kwa sababu wananchi watakuwa na afya nzuri na hilo ndio  lengo la Serikali.
"Iwapo usafi utadumishwa jamii itaishi kwa kuwa na afya njema itaepukana na maradhi ya mripuko na ndio azma ya Serikali yetu", alisema Waziri huyo.
Aidha amesema mji unapokuwa safi mazingira yanapendeza  hata watalii wataongezeka vijana watapata ajira na pato la Serikali litaongezeka.
Akielezea changamoto kwa jamii amesema bado haina uelewa wa kutia taka ndani ya sehemu maalum inayowekwa na manispaa na hili ndio linalosababisha kuzagaa kwa taka ndani ya mji.
Nae katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii  Zanzibar Abdullah Mohamed Juma amesema Nchi inategemea utalii kwani ndio uti wa mgongo hivyo tusafishe mji na kuweka mazingira yaliyo safi ili watalii waje kwa wingi.
Pia amesema taka ni rasilimali ambayo  inasarifiwa duniani na kwa hapa Zanzibar imeanza kukusanya chupa ambazo zishatumika kwa kusarifiwa na  nchi za wenzetu taka hufanyiwa baadhi ya mambo mengine kama vile mbolea na umeme.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaaya Wilaya ya Magharibi B Abdullah Saidi Natepe ameitaka jamii iwache tabia ya kutupa taka ovyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuchafua mazingira.
Zoezi hili la kusafisha mji ni endelevu lilianza Forodhani ,Nungwi, Jambiani na leo Mbweni na litaendelea kila sehemu katika mji wa Zanzibar kwa kushirikiana na Safisha Zanzibar na Wajamama katika kusafisha mji na baadhi ya vikundi vyengine.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.