Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza jambo alipotembelea kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivi ,Abdalah Ulega akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bidhaa za ngozi ya Kilimanjaro Mhandisi Masud Omari wakat wa ziara yake ya siku moja kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
Moja ya majengo ya kiwanda hicho yaliyojengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo .
Sehemu ya mashine zilizofika kwa ajili ya kusimikwa katika kiwanda hicho.
Awamu ya pili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakta ngozi ukiendelea katika eneo lililopo jirani na Gereza la Karanga mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akitizama mashine za kuchakata ngozi alipotembelea kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bidhaa za Ngozi ya Kilimanjaro Mhandisi Masud Omari akiumuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi moja ya mashine zitakazotumika katika kuchakata ngozi katika kiwanda hicho .
Mashine kwa ajili ya kuchakata Ngozi ambazo zinatarajiwa kufungwa katika kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro .
Na Dixon Busagaga ,Kilimanjaro
SERIKALI imesema ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sera
itayowezesha wanafunzi Mil 10 hadi Mil 20 wa shule
za msingi na Sekondari wanaoanza masomo yao kutumia viatu vitakavyozalishwa na
Kampuni ya bidhaa za Ngozi ya Kilimanjaro iliyopo mjini Moshi .
Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah
Ulega wakati ya ziara ya siku moja mkoani Kilimanjaro ambapo ametembelea mradi wa ujenzi wa viwanda vya kuchakata
bidhaa za ngozi vilivyopo chini ya kampuni ya Kilimanjaro Leather Industries Co
Ltd.
Akizungumza mara baada ya kujionea hatua za ujenzi
zilipofikia Naibu Waziri Ulega alisema katika kuunga Mkono Jitihada za Rais Wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk John Joseph Pombe Magufuli za
kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa viwanda, Mfuko Wa PSSSF umewekeza katika
Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Bidhaa za Ngozi Mkoani Kilimanjaro .
“Wito wangu tu ni kwamba taasisi za serikali ,ni muhimu sana
zikanunua bidhaa zetu sisi wenyewe tunazozalisha hapa sisi wenyewe hapa
nyumbani ,kwa mfano watu wengi hawajaamini kama vitu vinavyotengenezwa na
wajasiliamali wadogo wadogo na viwanda vyetu kama kweli ni ngozi .álisema
Ulega.
“Tunalo tatizo la bidhaa hizi za plastiki yaliyokarabatiwa
karabatiwa ,yameingia kwa wingi sana ,yamefanya hata wajasilia mali wetu hapa
zile bidhaa wanazotengeneza sio ngozi ,lakini zile ni ngozi na watanzania
tuamini kwamba zile ni ngozi.”aliongeza Ulega .
Alisema serikali inakusudia kuanza na watoto katika mashule ya msingi na Sekondari baada ya
kukubaliana na watungaji sera na viongozi katika wizara mbalimbali ambapo watoto
kati ya Mil 10 na 20 watapata viatu .
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hiki Mhandisi Masud Omar
amesema Kampuni hiyo pamoja na kampuni
za Italia ,TMC na ITALPROGETTI wapo kwenye taratibu za mwisho za kuanza kazi ya
kusimika mitambo na kwamba janga la
virusi vya Corona vimechangia kuchelewa kwa kazi hiyo.
“Ili kutekeleza agizo la Serikali, Kampuni ijulikanayo kwa
jina la “Karanga Leather Industries Co Ltd” (KLICL) ilianzishwa mnamo tarehe 30
Mei, 2017 kwa lengo la kuanzisha mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika
eneo la Gereza la Karanga, Moshi, Kilimanjaro kwa lengo la kuboresha kiwanda
cha ngozi kilichopo na baadae kujenga kiwanda kipya cha kisasa cha utengeneaji
wa ngozi na bidhaa zake. “alisema Mhandisi Omari .
Mhandisi Omari alisema kampuni hiyo ilianzishwa kwa ubia
kati ya uliokuwa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambao kwa sasa majukumu yake
yamechukuliwa na PSSSF pamoja na Jeshi la Magereza kupitia kampuni yake ya
Prisons Corporation Sole.
“Hatua ya kwanza (LOT 1) ya utekelezaji wa mradi
inayohusisha ujenzi wa kiwanda cha viatu yaani ujenzi wa jengo ya Ukataji na
ushonaji, umaliziaji, ghala na nyumba ya umeme yamekamilika na mmiliki ameanza
kuyatumia kwa matumizi ya kiofisi.
Alisema ujenzi huu umeenda sambamba na uwasilishwaji wa
mitambo ambapo mitambo yote kwaajili ya kiwanda hivi vilivyokamilika
vishawasili katika eneo la kiwanda huku zikisubiria wataalamu kutoka Italia
kuja kuzifunga.
Kiwanda kipya kimejengwa katika eneo la hekari 25 lililotengwa katika Gereza la Karanga Manispaa
ya Moshi Mjini huku uzalishaji wa kiwanda hiki ukitazamiwa kuzalisha jozi 4,000
za viatu kwa siku sawa na jozi 1,200,000 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment