Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni Jimbo la Mtoni Zanzibar.

Mgombea Ubunge Jimbo la Mtoni Zanzibar Ndg. Abdulghafar Idrisa Juma, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtoni wakati akitangaza sera zake katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya sharifumsa Mtoni. 

Wananchi wa Jimbo la Mtoni Zanzibar wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa jimbo hilo akinadi sera zake wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Sharifumsa Mtoni Jijini Zanzibar. 


Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Maudline Cyrus Castico amewataka wananchi kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi ili kizidi kuleta maendeleo endelevu na kudumisha amani nchini.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kuwatambulisha wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Mtoni katika nafasi ya Ubunge, Uwakilishi, Udiwani pamoja na Nafasi za Wanawake huko katika uwanja wa Sharifumsa.

Amesema kuwa wananchi wasipoteze kura zao kwa kuwatilia vyama vyengine wawachague viongozi wa CCM kwani ndio Chama pekee chenye kuleta maendeleo na kuwajali wananchi wake .

Nae Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo Abdulghafar Idrisa Juma alisema kuwa iwapo wanachama watamuamini na kumpa ridhaa ya kuwaongoza ataondoa changamoto zilizopo kwa kupambana na matatizo ya maji kwa kuwajengea visima vya maji ili kuwaondoshea usumbufu wananchi katika maeneo mbali mbali.

Alieleza kuwa ataimarisha vikundi vya akinamama kwa kuwajengea SACCOS ya Jimbo pamoja na vijana kuwafundisha mbinu bora za ujasiliamali kwa lengo la kuweza kujiajiri wenyewe .

Mgombea alisema kuwa atakusanya pamoja vijana wa boda boda kuwapatia mafunzo kupitia vyombo vya ulinzi na usalama jinsi ya kufanya biashara hiyo ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi na kufikia malengo ya kazi zao

Hata hivyo alifahamisha kuwa katika miaka mitano ijayo ataimarisha michezo katika jimbo hilo kwa kuweka ushindani wa ligi ili kuibua vipaji vingi vya wanamichezo.  

Aidha alisema  kuwa atashirikiana na Mwakilishi kumuunga mkono Mgombea Urais Dkt Husein Mwinyi katika kuimarisha sekta ya uvuvi ili kuwapatia ajira vijana na kukuza uchumi nchini.

Akiomba ridhaa mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mtoni Husein Ibrahim Makungu (Bhaa) alisema ataendeleza juhudi zake za kuwapatia maendeleo wananchi wake kwa kushirikiana na Mbunge huyo pamoja na kuilinda amani iliopo.

1 comment:

  1. iam a youth from mtoni want to engage my sef in bussiness but i dont have capital

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.