Habari za Punde

Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Kwa Tiketi ya CCM Mhe. Ummy Mwalimu - Amesema Atamaliza Migogoro ya Ardhi Jijini Tanga

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda wakati wa mkutano wake wa kampeni

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo

KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Mohamed Haniu akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa hadhara
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akiwasha moto kwenye mkutano huo


Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Usagara wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake wa kampeni

Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Usagara wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake wa kampeni
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Usagara wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake wa kampeni
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Usagara wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake wa kampeni

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuliongoza Jimbo hilo atahakikisha anamaliza migogoro ya ardhi iliyopo kwenye Jiji la Tanga ikiwemo Kata ya Usagara kwa kusimamia wenye haki kupata haki yao.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika mtaa wa Usagara Kijijini jirani na Magorofa ya Bandari.

Alisema kwamba anatambua kwenye Jiji hilo kuna baadhi ya maeneo kuna migogoro ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi hivyo ataishughulikia kwa kuhakikisha anasimamia haki ili mwenye kustahili apate haki yake.

“Ndugu zangu wana Usagara ninafahamu ipo migogoro ya ardhi hapa kwenu lakini na Tanga kwa ujumla hivyo nipeni ridhaa ya kuwa mwakilishi wenu tuweze kushughulika nayo kuhakikisha tunaimaliza”Alisema

Mgombea huyo alisema anafahamu kuna changamoto ya migogoro ya ardhi katika kata ya Usagara ikiwemo Usagara Kijijini ambapo alisema kwenye hilo atalifanyia kazi sambamba na kufanya maboresho ya wakazi wa Usagara kijijini.

“Kuhusu suala la umiliki wa nyumba kwa watu walionunua Nyumba za TBA na TPA niliwahaidi wana Usagara nitumeni bungeni suala lenu nitalikamilisha “Alisema Ummy Mwalimu.

Hata hivyo alisema kwamba ataendelea kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Usagara na Ujenzi wa barabara ya white rose ambayo hujaa maji wakati wa mvua.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.