Habari za Punde

DKT. TULIA AKEMEA VIPIGO KWA WANAWAKE

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akiangalia muonekano wa GBV APP iliyotengenezwa kwa ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam kulia mwenye koti ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.

Baadhi ya Wadau wakifuatilia masuala mbalimbali katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja pamoja na wanaharakati wa Mapambano dhidi ya Ukatili wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam wa pili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu. 

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekemea vitendo vya kupigwa kwa Wanawake na Watoto wa kike vinavyotokea katika Jamii.

 

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kampeni ya Siku 16 za kupinga Ukatili zikiongozwa na Kauli mbiu isemayo: Tupinge vitendo vya Ukatili: Mabadiliko yananza na mimi.

 

Dkt. Tulia amesema kuwa Jamii inatakiwa kuanza kutambua mchango wao katika juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya Ukatili vinavyotokea katika jamii.

 

"Jamii tuchukue hatua zaidi haya yanayotokea katika Jamii tunaweza tukayaponga na kuyakataa ndio maana tunasema mabadiliko yananza na mimi" alisema.

 

Aidha amesema Serikali imekusudia kuendelea kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa na Kitaifa ili kuhakikisha vitendo vya Ukatili katika jamii vinatokomezwa nankutoweka katika Jamii.

 

Pia Dkt. Tulia ameitaka jamii kuwapa fursa watoto wa kike sawa na watoto wa kike katika nyanja mbalimbali hasa katika kupata elimu na kusisitiza Jamii kuwaheshimu Wanawake na Watoto wa kike.

 

Akizungumzia utekekezaji wa Mipango mbalimbali ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau katika kuhakikisha vitendo vya ukatiki dhidi ya wanawake na Watoto vinatokomezwa nchini.

 

"Tutaendelea kutilia mkazo suala hili kwa nguvu zaidi na kutafuta namna mbalimbali za Mapambano ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto" alisema

 

Naye Mkurugenzi wa Wildaf Anna Kulaya amesema kuwa Wanawake wa vijijini na hasa wenye elimu duni wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili hivyo jitihada kubwa zinahitajika katika kuhakikisha Jamii hiyo unapata elimu ya kutokomeza vitendo vya kikatili.

 

"Utashangaa sana hata katika Vyuo na Vyuo vikuu kumekuwa na taarifa nyingi za uwepo wa vitendo vya kikatili kwa wanafunzi katika Vyuo hasa uwepo wa rushwa ya ngono" alisisitiza

 

Wakati huo huo Mhe. Tulia Ackson alizindua GBV APP maalum kwa ajili ya wananchi kutoa na kupata taarifa mbalimbali kuhusu vitendo vya ukatili ikiwemo elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

 

1 comment:

  1. Ni moja ya jukumu Kama kiongozi.ila tambua ya kwamba Kila Jambo linalotokea ndani ya jamii lisiangazie upande wa Nani anaepata madhara,bila kuangalia Nini na kwanini unyanyasaji unatokea.Ni kwamba lazma jamii iutambue Nini kiini Cha tatizo lenyewe.na lazma uelimishaji na uelekezaji ufanyike zaidi kwa wanaume au wakina baba.maana ata wanawake ni wanyanyasaji wakubwa Sana ktk maswala haha.na jamii ikitambua kuwaelimisha wanaume na waokukubaliana kwa moyo mmoja hayatatokea matatizo ya unyanyasaji huu.ila kwakua Sheria inamlinda Sana huyu mmoja bila kutenda haki sawia kijinsia basi hamjatibu tatizo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.